*Ni wa taasisi za umma, wanadaiwa sh. bilioni
1.4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo
ya maji ya DUWASA inayotoa maji yanayosambazwa katika Manispaa ya
Dodoma wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Mzakwe mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza apatiwe orodha ya wadaiwa
sugu wa taasisi zote za Serikali mkoani Dodoma ambao wamelimbikiza deni la sh.
bilioni 1.4 zikiwa ni bili zao za maji.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 2, 2016)
wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka Dodoma (DUWASA) mara baada ya kukagua utendaji kazi wa chanzo cha maji cha
Mzakwe nje kidogo ya mji wa Dodoma.
“Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za Serikali na
taasisi za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima yalipwe,”
amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya siku mbili ya kukagua
maandalizi ya Serikali kuhamia Dodoma, anatembelea sehemu mbalimbali za kutolea
huduma za jamii pamoja na kukagua miundombinu ya mkoa huo.
Aliutaka uongozi wa DUWASA na watumishi wote wahakakishe
wanaboresha huduma za upatikanaji wa maji hasa kwenye maeneo yanayopimwa
viwanja ili wananchi au wawekezaji wanaponunua viwanja wakute huduma hiyo ipo
na waanze ujenzi mara moja.
“Tumealika wawekezaji, nataka wajenge viwanda na mahoteli hapa
Dodoma, sasa wakikuta maji na umeme kwenye maeneo yao, itakuwa ni kichocheo cha
kuharakisha kazi za ujenzi,” amesema.
Pia amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi. Christina Mndeme
ahakikishe eneo lililo jirani na chanzo hicho cha maji halikaliwi na mtu yeyote
na linalindwa dhidi ya uchomaji mioto.
“Uchomaji moto uoto wa asili umeharibu vyanzo vingi vya maji. Ni
tatizo kubwa hapa nchini na halina budi kusimamiwa hadi liishe,” amesisistiza.
Amefikia uamuzi huo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi David Pallangyo kwamba kuna wananchi
wameanza kujenga na kufanya shughuli za kijamii jirani na chanzo hicho licha ya
kuwa walikwishaondolewa zamani.
Kuhusu wadaiwa sugu, Mhandisi Pallangyo alisema mashirika ya
umma na taasisi za Serikali ndiyo wanaongoza kwa kulimbikiza madeni. “Wananchi
wa kawaida wapo wanaodaiwa lakini deni lao siyo kubwa na hao tunawamudu,”
alisema wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema changamoto nyingine inayowakabili ni uchomaji moto
ambapo hivi karibuni uliwashwa moto na kuunguza baadhi ya nguzo za umeme ambazo
zinapeleka umeme kwenye chanzo hicho.
Alisema askari wa JKT Makutupora walisaidia kuzima moto huo ili
usifike kwenye mitambo mingine ya chanzo hicho cha maj
No comments:
Post a Comment