Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Brigedia Jenerali, Michael Luwogo akifafanua jambo kuhusu mashindano ya Waitara Trophy yatakaofanyika Novemba 19 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Captain Japhet Masai na Naibu Katibu, Kanali Rajabu Mohamed. (Picha na Francis Dande).
Mchezaji wa Klabu ya gofu ya Lugalo, Nicholous Chitanda akiwa katika mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya gofu ya Waitara Trophy yatakayoanza Novemba 19 na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kupitia kinywaji chake cha Johnnie Walker.
Na Luteni Selemani Semunyu
JAJI Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande anatarajiwa kuwa Mgeni
rasmi katika mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Generali Geogre
Waitara maarufu Waitara Trophy 2016.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi
la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wanaoandaa mashindano hayo Brigedia Jenerali
Michael Luwongo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam.
Brigedia Jenerali Luwongo alisema maandalizi yamekamilika na
yanatarajiwa kufanyika Jumamosi Novemba 19 na kushirikisha Wachezaji wa makundi
yote isipokuwa watoto huku klabu zote zikithibitisha kushiriki.
“Tumeshajiandaa vya kutosha na wadhamini wametuwezesha na mwitikio
mpaka sasa ni mkubwa na tayari wachezaji 150 wametibitisha kushiriki mashindano
haya yanayodhaminiwa na kampuni ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha John
Walker red label” Alisema Generali Luwongo.
Aliongeza kuwa mbali na Vilabu wenyeji klabu ya Lugalo ,Gymkhana
Dar es Salaam,Gymkhana Morogoro ,Gymkhana Arusha, Kili,na TPC Moshi ,na Mufindi
pia kutoka Arusha Mkuu wa majeshi Mstaafu Mirisho Sarakikya amethibitisha kushiriki
katika mashindano hayo.
Pia alisema Wanatarajia kuongea na Chama cha Golf Nchini ili kuona
namna gani baadhi ya Mashindano ya Ndani ikiwemo hili la Waitara kuwa na hadhi
ya Kimataifa kutokana na kuwa mashindano hayo na hamasa kubwa iliyopo.
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kapten Japhet Masai
alisema mashindano hayo yatakuwa ya Stroke play Net ambapo
yatatanguliwa na Wachezaji wa Kulipwa na Wachezaji wasaidizi siku ya Ijumaa
Novemba 18 huku siku inayofuata yakifanyika kwa makundi yaliyosalia.
Naye Meneja wa mawasiliano wa Serengeti Abbas Abraham alisema
maandalizi ya zawadi ikiwemo ya Vikombe yamekamilika na wanachosubiri ni zoezi
la kukabidhiwa kwa Washindi.
Mashindano ya Kombe la Waitara yanayofanyika kila mwaka ikiwa
ni kumbukumbu ya kutambua mchango mkubwa uliotolewa na mkuu huyo wa majeshi
katika kuanzisha Uwanja wa Golf wa Lugalo Mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment