HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 10, 2016

MOTO MKUBWA WATEKETEZA BOHARI LA KAMPUNI YA 7 GENERAL ENTERPRISES MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

Hivi ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.
 Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari
 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka moto utakapozimwa kabisa 
Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika
 Mmoja wa waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa.
 Moja ya Gari la zima moto likiwa linawahi eneo la Tukio kusaidia kuzima moto
Zima moto wakiendelea na shughuli ya kuhakikisha moto unazimika katika Bohali hilo
 Moto ukiendelea kuteketeza Bohari hilo lililokuwa la kuhifadhia mataili
 Pamoja na watu kupewa tahadhali ya Moto mkubwa uliokuwa unawaka lakini bado walikuwa wakiongezeka kushuhudia tukio hilo.
 Katika juhudi za kuhakikisha moto huo unazimika kabisa magari ya kila aina yanayobeba maji yalichukuliwa kuongeza nguvu za kuzima moto huo. Picha na Freddy Njeje.

No comments:

Post a Comment

Pages