Mkazi
Usagara Tanga, Joseph Kimani, akiangalia majina
ya askari wa Uingereza na India waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 270 waliuwawa Tanga wakati wa vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1914.Majina hayo yamehifadhiwa na tume ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth War Graves Cammission) (CWGC)
ya askari wa Uingereza na India waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 270 waliuwawa Tanga wakati wa vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1914.Majina hayo yamehifadhiwa na tume ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth War Graves Cammission) (CWGC)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
TUME ya Jumuiya ya Madola inayosimamia Makaburi ya Vita vya Kwanza vya Dunia (CWGC) inatarajiwa kuzindua hapa makaburi mapya ya askari wa Kihindi waliokufa katika vita hivyo vya kwanza vya dunia.
Akizungumza na waandishi habari jijini Tanga jana , Ofisa ufundi wa Jumuiya hiyo, Daniel Achini, alisema uzinduzi huo utafanyika mwezi Novemba 11, 2016.
Achini alisema uzinduzi huo utafanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo ya CWGC, Victoria Wallace ukishuhudiwa na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cook na Balozi wa India, Sandeep Arya.
Sherehe hizo
pia zitahudhuriwa na Balozi wa Ujerumani, Egon Konchake na
viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la
Tanga.
Alisema makaburi hayo mapya yapatayo 62 yamezikwa miili ya askari wa Kihindi waliokufa vitani katika eneo la Jasin kati ya Januari na Julai, 1915.
Makaburi
hayo yamejengwa maeneo ya Usagara na Jasin, karibu na jiji.
Kumbukumbu
ya makaburi ya Wahindi na yale ya Usagara yaliyoko hapa Tanga
ni sehemu tu ya makaburi mengi yanayohudumiwa na Tume hiyo ya CWGC.
Ofisa huyo
alieleza kuwa makumbusho ya Jasin, ulikuwa ni mji wa mbele wa
kujihami katika pwani ya kaskazini ya mji wa Tanga na ambao ulichukuliwa na
Wajerumani mwezi Januari, 1915.
Alisema
vikosi vya Jind na Kashmiri ndivyo vilivyoulinda mji, ambao
ulitekwa na kuchukuliwa tena na vikosi vya wanajeshi 2,000 wa Kijerumani tarehe
18 Januari, 1915.
Makumbusho
ya makaburi ya Tanga ambayo yapo katika eneo la Usagara,
yanahifadhi kumbukumbu ya vifo 394 vilivyotokea katika vita vikali
vilivyopiganwa katika mji wa Tanga kati 1914 na 1916 baina ya mataifa makubwa
ya Uingereza na Ujerumani.
Achini
alifafanua kwamba moja ya kazi muhimu ya Tume hiyo barani Afrika
ni pamoja na kutunza makaburi na kumbukumbu za vifo zaidi 190,000 vilivyotokea
katika vita vya kwanza na pili vya dunia katika nchi zaidi ya 40 zilizopo
Afrika.
"Nchini
Tanzania, tunavikumbuka vifo zaidi ya 55,000 vilivyotokea
katika vita vyote katika viwanja 12 vya makaburi", alidokeza Achini.
Alitaja baadhi ya maeneo ya makaburi yanayohudumiwa na
CWGC yanapatikana
Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa na Moshi
Zanzibar.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment