HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 08, 2016

PPF YAANDIKISHA MAMIA YA WAPANDA BODABODA KUWA WANACHAMA WA MFUKO HUO KUPITIA MPANGO WA WOTE SCHEME

 Baadhi ya wapanda boda boda kati ya 250 waliojiunga na Mfuko wa Pnsheni wa PPF kupitia mpango wa "Wote Scheme wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha mfano wa kadi za kujiunga na mpango huo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, Novemba 7, 2016.
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Mkemwa William Faustin.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MFUKO wa Pensheni wa PPF umeendelea na kampeni yake ya kuandikisha wanachama wapya kupitia mpango wa “Wote Scheme”, unaohusisha wafanyakazi walio katika sekta rasmi na wale waliojiajiri wenyewe ambapo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, zaidi ya waendesha bodaboda 250, kutoka wilaya ya Temeke, walijiunga na mpango huo.

Katika uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe-Yanga, wilayani humo Novemba 7, 2016, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwakabidhi kadi za uanachama wa Mfuko huo baadhi ya waendesha bodaboda hao.

Akizungumza baada ya zoezi hilo la kuwakabidhi kadi hizo, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele alisema, zoezi la kuandikisha wanachama wapya wakiwemo hao wa bodaboda, litakwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama ambayo itafanyika kwenye wilaya za Ilala, na Kionondoni pia.

“Tunatoa wito kwa, wananchi wote, wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, bodaboda, machinga, kujiunga na mpango huo ambao una faida nyingi ikiwemo kujipatia bima ya afya, mikopo ya elimu na mafao mengine mengi.” Alifafanua.

 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Lowowa Emmanuel Julius
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Rubamande Ratifa Ally
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya PPF, Bw. Shinne Gustaph Patrick
 Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akimpongeza mwanachama mpya wa PPF, ambaye ni dereva wa Bodaboda, Bw.
Mkemwa William Faustin
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda  ya Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Mroto wakati akiwasili. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala, Salum Hamduni
 Kamanda wa polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Temeke, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, (ASP), Solomon Mwangamilo, akizungumza jambo na Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), Bw. Yahya Charahani.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala, Salum Hamduni.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilaya ya Temeke, ASP, Solomon Mwangamilo.
 Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Mkuu wa Kituo cha Polisi, (OCS), cha Mabasi ya Mkoa, Ubungo Bus Terminal, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, (ASP), Sarah Bundala
 Polisi wa usalama barabarani wakiingia kwa maandamano kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga
 Askari wa usalama barabarani akiyaelekeza magari yaliyoshiriki kwenye maanadamano siku ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam, viwanja vya Mwembe-Yanga
 Waendesha Bodaboda wakiwasili kwa maandamano kwenye viwanja hivyo
 Mwanachama mpya wa PPF, ambaye ni mwendesha bodaboda, Ratifa Ally, (kushoto), akibadilishana mawazo na Maafisa wa PPF Kanda ya Temeke, Elizabeth Chambiri, (kulia) na Donald Maeda.
 Brass Band ya polisi ikiongoza maandamano
 Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, (kulia), akipatiwa malezo ya shughuli za Mfuko wa Pensehni wa PPF, kutoka kwa Msimamizi wa Kanda ya Temeke, Sospeter Lyimo, (wapili kushoto). Kulia ni Bi. Elizabeth Chambiri
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Jannet Ezekiel, akimpatia maelezo Afisa huyu wa polisi kuhusu mpango wa Wote Scheme, ambao Polisi nao wanaweza kujiunga nao
Mwanachama mpya akisajiliwa kujiunga na Wote Scheme.

No comments:

Post a Comment

Pages