HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 10, 2016

TTCL YAWAFUATA WATEJA MITAANI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

   KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, leo imeanza Kampeni ya kuwafuata wateja wake mitaani ili kuzungumza nao, kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaunganisha wateja hao katika huduma mbali mbali za TTCL.

 Kampeni hiyo imeongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri W. Kindamba na kusaidiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wafanyakazi wa TTCL waliosambaa katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam.

 "Huu utakuwa ni utamaduni wetu, tutawafuata Wateja popote walipo, tutawapa taarifa za huduma zetu bora na nafuu, tutawasikiliza na kufanyia kazi maoni yao. 

Tunataka kuwahakikishia Wananchi kuwa, hii ni TTCL Mpya, Shirika lao la kizalendo limerejea katika nafasi ya mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini Tanzania.

 Watumie huduma zetu, waone tofauti, wapate ubora na viwango vya juu kabisa", amesema Bw Kindamba. Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL Bw Peter Ngota amesema, TTCL inawaletea wateja wake Ofa MPYA kabambe kwa ajili ya Simu ya Mezani inayotoa uhakika wa mawasiliano kati ya Wanafamilia. Kwa Mteja atakayeongeza salio la shilingi 23,000/- atapata ofa ya Simu Bure pamoja na ofa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure. Afisa Mkuu Masoko na Mauzo wa TTCL, Bw Peter Ngota akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Afisa Mkuu Masoko na Mauzo wa TTCL, Bw Peter Ngota akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

Pages