Baadhi ya watu wakiwa wamekusanyika baada ya mtuhumiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Mtuhumiwa wa tukio la kumchoma moto mpenzi wake, Omari Said Omari (24)
Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar limefanikiwa kumtia nguvuni na kumuweka korokoroni kijana Omari Said Omari (24) ambaye anatuhumiwa kumshambulia na kumuumiza vibaya kwa kumchoma moto bi Samira Abas Amin (26) huko mkoa wa Kusini Unguja.
Akizungumza na Waandishi wa habari huko Afisini kwake kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nasir Ali alieleza kuwa walifanikiwa kumkamata kijana huyo baada ya purukushani kubwa kati ya Jeshi hilo na kijana huyo katika eneo la Darajani mnamo muda wa saa tano Asubuhi ambaye alikuwa njia kukimbilia Airport kwa ajili ya kutoroka.
“Tuliweka mtego wetu wa kitaalamu kwa kushirikiana na raia wema ambao ndio uliotufanya tufanikiwe kumkamata muhalifu” alieleza kamanda Ali.
Alieleza kuwa kwa taarifa walizozipata mtuhumiwa huyo wa uhalifu alikuwa na lengo kukimbia lakini alidai walijipanga kitaalamu kwa kushirikiana na raia wema walifanikiwa kumkamata akiwa ndani ya Gari aina ya vits (Z 853 GJ).
“Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba kabla ya kutokea hujuma hiyo wawili hao walikua wapenzi ambao wakiishi katika Nyumba moja katika kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini” alieelza Ali.
Alieleza upelelezi unaendelea na ukishakamilika watampeleka Mahakamani Mttuhumiwa huyoo ili kile kinachodaiwa kupata ukweli.
Kwa taarifa za watu wa karibu wa wapenzi wa wawili hao wanaeleza kuwa watu hao walikua wa penzi kwa muda mrefu.
Likiwa penzi likionekana kuingia Dosari katika wiki moja nyuma Omar Said Omar aliweza kumuona aliyekuwa mpenzi wake na Mwanamme mwengine akiwa Disko na kumchukua kwa Nguvu hadi walikokuwa wanalala na kuamua kutia Mafuta kisha kumchoma moto.
Wakati kijana huyo akitiwa nguvu kwa Upande wa Samira badon yuko katika Hospital ya Makunduchi Mkoa wa Kusini kwa ajili ya kupata matibabu akionekana akiwa katika hali isiyoyakuridhisha.
Baada ya tukio hilo la Jeshi la Polisi kkufanikiwa kumkamata kijana huyo Jumuiya ya Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) kimelielezea tukio hilo kuwa la kutia moyo katika jitihada za kutokomeza udhalilishaji wa kijinsia.
Mratibu wa Miradi katika Jumuiya hiyo bi Asha Abd alisema kama hatua kama hizo zitachukuliwa dhidi ya wadhalilishaji basi wanaweza kupiga hatua ya kuzui.
“Kumbe inawezekana hemu tutimizeni wajibu wetu kupiga vita ukatili wa klijinsia na udhalilishaji wanawake na watoto” alieleza Bi Asha.
No comments:
Post a Comment