HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 31, 2016

Wafanyabiashara wa mboga mboga Pemba walia na Baraza la Mji

Na Talib Ussi, Zanzibar

WAFANYABIASHARA wa mbogamboga kisiwani Pemba wamesema, wanasikitishwa na kitendo cha kupandishwa kodi kila Baraza la mji linapojisikia.

Sambamba na hilo walieleza kuwa  Baraza  hilo huamua tuu bila kuwepo mashauriano nao na hasa katika kubadilisha kwa mikataba wakiwa katikati ya mwaka, jambo ambalo linawakwaza katika kuendelea na biashara zao.

Waliyasema hayo ofisi za baraza la mji chake chake wakati wakikao cha kupokea taarifa ya mikataba mipya pamoja na kodi mpya kwa mwaka 2017, huku wakilalamikia matatizo mbalimbali yanayowakabili.

Walieleza hayo mbele ya maofisa wa baraza hilo kuwa, kitendo cha kupandishwa kodi kiholela na kubadilishwa kwa mikataba katikati ya mwaka ni uonevu mkubwa unaotendeka kiupande wao, ambapo hupelekea kuzorotesha maendeleo yao ya kibiashara na itafikia muda waamue kuacha kufanya kazi hiyo.

Walieleza kuwa, watafikia mahali biashara itawashinda kuendelea nayo kutokana na kulichumia baraza hilo pekee bila ya wao kupata faida yoyote ile.  

Akizungumza mbele ya hafla hiyo Mzee Maulid Issa Salum alisema, hali hiyo inawasikitisha sana, kwani hapo awali walikuwa wanalipishwa shilingi elfu 25,000 kwa mwezi kama ada ya kodi ingawa kwa sasa wanalipishwa shilingi elfu 50,000 kwa mwezi ambayo ni mara mbili yake.

“Mfano ni wauza mboga waliopo soko la Chake Chake tumekuwa tukinyanyaswaa vibayaa kama vile sisi wageni katika nchi hii” alieza mfanya biashara huyo.

Alidai kuwa, baraza kwa sasa halina mashirikiano yeyote na wafanya biashara hao tofauti na hapo awali alipokuwepo mkuregenzi aliyoondoka madarakani bwana Seif  Shaaban, kutokana na kufanya maamuzi peke yao ikiwamo mikataba hiyo na kulitaka baraza liwapunguzie kodi.

Nae Juma Salum Abdallah  alisema kuwa, kuwachiwa wafanyabiashara holela mbele ya soko ambao hawakati leseni kunawaumiza mno nakuwarejesha nyuma kwani biashara zao zimekuwa hazitoki na kuwasababishia hasara za maksudi na kulitakaa baraza liwaondoshe watu hao ili kunusuru biashara zao.

“Halafu baraza hili linamaneno ya kejeli  kabisa eti asiyeweza kulipa kodi na aondoke sasa tunauliza  huo ndio utendaji au ndio uongozi mpaya wa SMZ” alieelza Abdallah ambaye anauza biashara ya Mchicha.

Alieelza kuwa licha ya kupandisha kodi zoote hizo katika soko hilo hakuna huduma hata moja ya kijamii, kama vile maji safi na eneo maalum la kuweka taka taka.

Akijibu masuali hayo Mzee wa baraza, Omar Suleiman Omar alisema, wakati umebadilika na gharama za maisha zimepanda hivyo wanapaswa kufanya wanayofanya na kuahidi kushungulikia baadhi ya kadhia ikiwemo kuutambuwa uongozi wa kamati ya wafanyabiashara hao ambao wamelalamika kuwa hata walipoiyunda haikuwa yenye kuzingatiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages