HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 31, 2016

Wakulima wa Nyanya Kisiwani Pemba walilia soko

Na Talib Ussi, Zanzibar

Kila anayekwenda shamba na jembe hua anamatumaini ya kupata faida katika uwekezaji kupitia ardhi.

Mara nyingi watu hasa wanyonge hukimbilia katika kilimo ili waweze kujikwamua na hali ngumu inayowakabili kimaisha.

Lakini matumani hayo yamekuwa kinyume kwa wakulima wa mboga mboga kisiwani Pemba kwa kile walichokieleza kuwa wanalima katika hali ngumu lakini hawana soko la uhakika la kuuza mazao yao jambo ambalo wanshindwa kutatua shida zao.

Mwaandishi wa makala hii alitembea katika ameneo mbali mbali kisiwani humo kama Vile Wingwi, Mchanga Mdogo na Mjini Kiuyu kwa upande wa kaskazini Pemba na Pujini kwa Kusini mwa kisiwa hicho na kujionea wazi wazi neema ya kilimo hicho hasa kilimo cha Nyanya kilivyoenea kila kona.

Jambo la kuvutia wengi ambao wanajishuhulisha na kilimo hicho ni vijana wa aina zote yaani wa kike na kiume.

Akizungumza na mwandishi wa wa makala hii akiwa shambani huko Wingwi Njuguni hidaya Ali Juma (32) alieleza kuwa alihangaika kwa miaka mingi kutafuta kitu cha kufanya ili aweze kujikwamua na hali ngumu inayomkabili.

“Shamba langu unaliona hili lina ukubwa wa akar moja na nusu na Alhamdulillah Nyanya zimezaa vizuri lakini wanunuzi ni wachache jambo ambalo nashindwa hata kufikia mlengo yangu na kutatua shida zangu” alieelaza hida.

Alieelza kuwa huu ni mwaka wa 7 yumo katika kiliomo hicho lakini bado hajapatika mafanikio hasa yale ambayo alikuwa amaejiwekea, kutokana na bei bidhaa hio kuonekana kushuka siku hadi.

“Kiukweli mwaka huu mambo yamekuwa magumu sana kwani ukiangalia bei za Nyanya zimekuwa chini kulingana na miaka iliyopita ambapo ndoo moja aliweza kuuza kwa 5000-4000, tofauti na miaka iliyopita ambapo ndoo moja waliuza 10000-8000” alieelza Hidaya.

Alieleza kuwa jambo kubwa linalopelekea bidhaa zao kushuka bei ni uingizwaji wa bidhaa kama hizo kiholela kutoka njee ya Zanzibar na bidhaa zao kuaza kuharibika shambani.

“Kweli zamani tulikua hatuzalishi bidhaa kama hizi ndio wafanmyabiashara wakawa wanaenda nje ya Visiwa vyetu kuchukua bidha hiyo, lakini sasa tunazalisha naona hakuna haja ya kuruhusu kuingizwa bidhaa ambazo za sisi tuna uwezo nazo” alieelza Bi hidaya.

Chumu Hasan Jabu (39) mkulima wa mboga mboga,katika bonde la kijiji cha Mjini kiuyu wilaya ya wete Mkoa wa kaskazini Pemba yeye amekuwa tofauti na bi Hidaya kwa alijinasibu kuwa amepata mafanikio makubwa.

Alisema kilimo kimeweza kumsaidia kuendelea kuwasomesha watoto wake skuli, ikiwemo kulipia ada, kununua mabuku, yunifom hata kuweza kumalizia banda lake ambalo kwa sasa anaishi.

“Mimi zaidi nalima bidhaa tofauti lakini ninchokitegemea ni Nyanya kwani ndio nimeiona ina matumizi ya kila siku na watu wengi wanapendelea kuitumia” alieleza Chumu.

Alieleza kuwa kwa upande wake aliweza kuuza ndoo moja ya Nyanya kati ya 12,000-10,000/=, ambapo aliweza kuvuna ndoo kwa msimu huu.

“Kiukweli nimeingia katika kilimo kwa kuona watu wengi wamepata tija nzuri katika mazao hasa haya ya mboga mboga” alieleza Bi zume Omar mkulima wa mboga mboga kutoka kijiji cha Pujini wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema licha ya kuwa ni mara yake ya pili kuingia katika kilimo hicho, lakini tatizo kubwa kwakwe ni ukosefu wa soko la uhakika hali ambayo inaweza kuvunja ndoto zake za kufikia maendeleo kupitia sekta ya kilimo.

“Kwa siku nilikuwa navuna ndoo 4-5, ndoo ya Tungule moja 5000, aa lakini kwa sasa ndugu yangu hali imekuwa tofauti hasa mwaka huu hasa na kila kukicha tunapandishiwa makodi yasio taa na maana” alieleza Bi zume.

Alieleza katika kile alichokipata kupitia bidhaa yake hiyo ameweza kununua Cherahani mbili na kufanyakazi nyengine za ushoni na huku kilichobakia akiwaendeleza watoto wake kimasomo.

Asha Khamis Omar (36) mkulima alisema baada ya kupata mafanikio makubwa katika kilimo cha Nyanya, sasa mikakati yake ni kupanda Vitunguu Maji, Matango na Matikiti maji, ili kuimarisha zaidi kilimo chake kutokana na vitu hivyo kuonekana kuwa na bei yenye kuridhisha.

“Nimegundua kwa sasa watu wengi wameingia kwenye kilimo cha Nyanya sasa mimi na hisi ni wakati wa kubadilisha muelekeo ili kuweza kupambana na maisha na upatikanaji wa soko” alieelza Asha.


Hassan Said Hassan (33) mkulima wa Tungule ( NYanya) alisema kilimo ndio kitu pekee kitakachompatia mtu tija na kuweza kujikwamua na maisha kwa kile alichodai kama mtu atakishuhulikia na kufuata maelekezo basi kimpatia anayoyahitaji.

“Lakini kwa kwetu tatizo kubwa ni kukosekana Viwanda vya kusindika haya mazao na kuwachiwa huru wafanyabiashara kuingiza Bidhaa ambazo sasa tunazlisha vizuri humu Visiwani mwetu ambazo zinarudisha juhudi zetu za kujikwamua na umasikini”

Kwa upanmde upande mwengine wakulima hao walieleza kuwachamaoto kubwa zinazowakabili ni kuwa na mtaji mdogo ambao nunawakosesha kuwa na mambo muhimu katika sehemun za uzalishaji.

Walieleza kuwa kama hakuna hakuna Mvua basi mazao yao inakuwa ngumu kutokana kushindwa na uwezo wa kumiliki mabwawa na kuhifadhia maji kwa ajili ya kuwamgilia mazao yao.

Walieleza kutokana na kukosa mbwawa katika maeneo ya mashamba wanalazimika kuchukua maji kwa kichwa kila siku tena yenye umbali karibu nusu kilomita.

Wakulima hao wa mboga mboga wameiyomba Serikali kuwasaidia kwa kuwapatia vifaa vya kumwagilia maji, ili kufikia malengo yao ya kuingia katika kilimo cha biashara.

Wakulima hao walisema kama viwanda vingekuwepo basi vingeweza kuwasaidia sana katika shihuli zao za kilimo, kwani msimu uliopita baadhi ya bidhaa zimeweza kukosa soka na kuharibika katika mashamba yao.

Katibu wa kikundi cha Tunasonga mbele Mchanga Mdogo wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, kinachojishuhulisha na ukulima wa mboga mboga na ufugaji wa mbuzi Seif Ali Abdalla alieelzea kusikitishwa na soko la bidhaa zao na kudai ni kikwazo kikubwa cha mafanikio yao.
Abdallah  alisema licha ya kujikusanya kwao lakini bado soko limekuwa ni tatizo kubwa kwao.

Naye aliuungana na wezake walioitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupiga marufuku uingizaji wa bidhaa za mboga mboga kutoka nje za Zanzibar.

Suala hilo la kutaka kuzuia bidhaa hizo kuingizwa hapa Visiwani lilipata nguvu pale mwenyekiti wa wenyeviti wa kamati za baraza la Wawakilishi Hamza Hassani Juma aliyetumia muda mkubwa katika vikao vya bara hilo lililoaghrishwa hivi karibuni kuiomba Serikali kufikiria kupiga marufuku bidhaa hizio kwa madai kuwa Zanzibar sasa inajiweza.

“Mheshimiwa Spika tumefanyakazi kubwa ya kuwashawishi wananchi wetu wajushuhulishe na kilimo na wito wameuitikia lakini wanalalamika kwa serikali yao kuruhusu bishara kama wanazolima wao kuingia nchini amba wanasema linawinyima soko wao” alieelza Juma.

Alieleza kuwa wakati umefika kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa mbali mbali hasa zile za mboga mboga alidai kuwa uzalishaji Unguja na Pemba umekuwa mkubwa.

Lakini akionekana kuukataa ushauri huo Waziri wa biashara Amina Salum Ali alieleza kuwa bado uzalishaji wanaozalisha wananchi wa Zanzibar uko chini na kudai hata uhifadhi siwa kuridhisha.

Ni kweli tumefikia kiwango kizuri cha uzalishaji lakini bado hakijawa na uwezo wa kuzuia bidhaa kutoka nje ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages