HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 27, 2017

HAKUNA MABADILIKO YA UTAWALA ZANZIBAR: BALOZI SEIF IDI

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu katika hafla ya makabidhiano ya  vifaa vya Michezo kwa Timu zinazoshiriki Mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja hapo ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar. (Picha na OMPR – ZNZ).
 Baadhi ya Wanamichezo wa Timu za Majimbo wakifuatilia hafla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zao hapo Ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
 Kikundi cha Utamaduni cha CCM Mkoa Mjini Big Star kikitoa burdani wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa  Makamuj Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Balozi Seif akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa Kusini Unguja Mh. Mohamed Raza ambae ia ni mdhamini wa mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja nje ya ukumbi wa CCM Aman Mjini Zanzibar.

                     ZANZIBAR                        

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Idi amewaasa wana CCM na wananchi wote Nchini kuacha tabia ya kuhamanika kutokana na uvumi unaoenezwa  mitandaoni kwamba yapo mabadiliko ya utawala wa Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Alisema Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba uchaguzi Mkuu wa Zanzibar  umekwisha kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na kuwataka kuelekeza nguvu zao katika kusimamia mirai yao ya maendeleo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akitoa salamu kwenye Hfla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu za Soka zitakazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo hapo ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.

Aliwatanabahisha wale wote wanaoendeleza kasumba ndani ya mitandao ya Kijamii kwa kuwadanganya Wananchi kwa makusudi waendelee kuvumilia na kustahamili hadi utakapofika uchaguzi mwengine Mkuu wa Mwaka 2020.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwa jumla kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ataendelea kuviongoza Visiwa vya Unguja na Pemba hadi utakapofanyika uchaguzi mwengine mwaka 2020 kama Katiba ya Zanzibar inavyoeleza.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
27/2/2017.

No comments:

Post a Comment

Pages