HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2017

Kilimanjaro Premium Lager yafurahishwa Kili Marathopn 2017

Na Mwandishi Wetu


Mdhamini mkuu wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ameeleza kufurahiswa na idadi ya watu waliojiokeza katika mbio hizo siku ya Jumapili na kuyafanya yawe moja ya mashindano makubwa Tanzania kwani zaidi ya watu 10,000 walijitokeza kukimbia na kushangilia.

Akizungumza mara baada yam bio hizo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,Pamela Kikuli alisema umati uliojitokeza katika mbio hizo ni wa aina yake na ni ishara kuwa riadha inakuwa.

“Nia yetu kama wadhamini ni kuona riadha ya Tanzania inafikia kilele cha mafanikio na tumeliona hili kwani marathon yetu inakuwa mwaka hata mwaka,” alisema.
Alishukuru waandaaji Wild Frontiers, waratibu kitaifa Executive Solutions, Chama Cha Riadha Cha Mkoa wa Kilimanjaro jeshi la polisi, utawala wa mkoa na wanariadha wote kwa kufanikisha mbio hizo.

“Mbio hizi zimesaidia kuleta biashara kwa wafanya biashara wa Moshi katika siku chache hizi kwani wageni walitumia huduma na bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukuza utalii,” alisema na kuongeza bia ya Kilimanjaro Premium Lager 375ml imepokewa vizuri na wakazi wa Moshi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugataalisema tangu waanze kudhamini mbio hizi miaka mitatu iliyopita za mwaka huu zimefana zaidi kwani mamia walijitokeza na kikubwa zaidi mshindi wa mbio hizo, Emmanuel Giniki ni Mtanzania.
“Haya ni mafanikio makubwa mno na tunawashukuru waandaaji kwa kazi kubwa walioifanya mbio zetu za 21km zinazidi kukua mwaka hata mwaka na tutaendelea kushirikiana na Kilimanjaro Marathon.

Mkurugenzi wa Masoko wa GAPCO Tanzania Caroline Kakwezi alisema washiriki wa mbio za kilomita 10 kwa walemavu  walifurahia utaratibu wa mwaka huu ambapo GAPCO ilitoa usafiri, malazi na chakula kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na usafiri kwa wale kutoka Arusha na Moshi.

“Tunatarajia kuwa na mashindano makubwa zaidi mwakani kwani mwaka huu tulifanya mchujo kwa kushirikiana na Kamati ya Paralimpiki Tanzania na kufanya mbio ziwe na ushindani mzuri,” alisema.

Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Oscar Shelukindo alisema alifurahishwa na idadi ya watu waliojitokeza kukimbia mbio za kilomita 5kwani ni ishara kuwa watu wanajali afya zao.
Wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2017 ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo 21km, GAPCO 10 km-kwa walemavu, Grand Malt-5km Fun run. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.
 Mshindi wa kwanza wa Kilomita 21 ya Kilimanjaro Marathon yaliyozaminiwa na Tigo, Mtanzania, Emmanuel Giniki, akimaliza mbio wakati wa mashindano yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro kwa udhamini wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mshindi wa kwanza wa Kilomita 10 ya Kilimanjaro Marathon kwa walemavu yaliyodhaminiwa na Gapco, Chales Mihambo , akimaliza mbio wakati wa mashindano yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro kupitia bia ya Kilimanjaro.
 Mshindi wa kwanza wa Kilomita 42 Moses Hengintti, akimaliza mbio wakati wa mashindano yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
 Mshindi wa kwanza wa Kilomita 21 wanawake ya Kilimanjaro Marathon, Grace Kimanzi , kutoka Kenya  akimaliza mbio wakati wa mashindano yaliofanyika Moshi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo, Profesa, Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi zawadi Mshindi wa kwanza wa Kilomita 21 kwa Wanaume ya Kilimanjaro Marathon , Emmanuel  Giniki, Mtanzania  akimaliza mbio wakati wa mashindano yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Mshindi wa kwanza wa Kilomita 42 Wanaume Kilimanjaro Marathon, Moses Hengitti akimaliza mbio wakati wa mashindano yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mmoja wa washiriki wa mbio za Kilometa 21 za Kili Marathon, Albert Maya  akiwa amepozi kwa picha huku akiwa ameshika medali yake ya Shaba, bio hizo zilifanyika mjini Moshi.

Washindi wa mbio za kilomita 21 zilizodhaminiwa na Tigo kwenye Kili Marathon wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages