Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani kutoka kwa msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni .Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi
Hamad Masauni, akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed
Mpinga, ambae pia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na
msamaria mwema,Tahir Othman (hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini
kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment