HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 24, 2017

Kili Marathon yaleta msisimko Moshi

Washiriki wa Kilimanjaro Marathon 2017 wakijisajili katika Hoteli ya Keys Mjini Moshi. (Na Mpiga Picha Wetu).

Na Mwandishi Wetu

MJI wa Moshi tayari umepata msisimko mkubwa huu watu wakianza kufurika kufuatia mbio za Kilimanjaro Marathon 2017 ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapiii Februari 26.

Tayari hoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu nyingine zinazotoa huduma mbalimbali zimeonekana kuwa na watu wengi kuashiria mambo yameiva huku zoezi la kujisajili likifikia tamati Jumamosi saa sita mchana.

“Kwa kweli msisimko uliopo Moshi sasa hizi ni wa aina yake na ndio maana sisi tukiwa wadhamini wakuu tunapata nguvu ya kuendelea kudhamini mbio hizi kwani ni kubwa na huwaleta watu wengi pamoja,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa mbio hizo.

“Mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi na ni matumaini yetu kuwa watu watajitokeza kwa wingi. Tumejiandaa vizrikabisa kwani baada yam bio kutakuwa na burudani kutoka kwa Joh Makini na Dogo Janja na yote haya yataenda sambamba na bia zetu ambazo sasa tunauza kwenye chupa mpya za ujazo 375ml kwa tsh 2000 tu,”

Naye Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata alisema wao kama wadhamini wa mbio za kilometa 21 wamejiandaa vizuri kabisa. “Zoezila usajili limeenda vizuri na bila shaka mbio hizi zimekuwa maarufu mno kwani watu wengi wamepata muamko wa kushiriki,” alisema na kuongeza kuwa msisimko uliopo sasa hivi Moshi ndio huwafanya watu wengi kuvutiwa.

Alisema watakuwa na promosheni mbalimbali ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kukutana na wateja wao kupitia mbio za Kilimanjaro Marathon. “Tunaomba washiriki watembelee mabanda yetu katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika Moshi,” alisema.

Meneja Masoko wa GAPCO Caroline Kakwezi alisema washiriki wao wote wa mbio za kilometa 10 kwa walemavu, wanatarajiwa kuwasili kufikia Jumamosi jioni tayari kwa mashindano. “Tumewalipia washiriki kutoka Dar es Salaam malazi, usafiri na chakula na wale kutoka Arusha na Moshi tumewalipia usafiri ni matumaini yetu kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na ushindani mkubwa kwani washiriki hawa wote walipatikana kwa njia ya mchujo zoezi ambalo liliendesha na Kamati ya Paralimpiki Tanzania.

Meneja wa Grand Malt, Oscar Shelukindo alisema kwa upande wa mbio za kilometa tano (fun run) maandalizi yote yamekamilika na msisimko ni mkubwa. “Washiriki wetu watapata nafasi ya kunywa Grand Malt ambacho ni kinywaji safi kwa afya,” alisema na kuongeza kuwa wanatarajia washiriki wengikushinda mwaka jana.

Wadhamini wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

Mbio za mwaka huu zinatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya chuo cha Ushirika Moshi (MuCO) kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Pages