Mkurugenzi wa Elimu katik Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Suleiman Yahya akionyesha aina ya kitabu cha kiengereza ambacho kitatumika katika kuwafundisho wanafunzi wa Sukuli Zanzibar kuazia darasa la 1 hadi la 4 shuhuli hiyo ilifanya Ngome Kongwe, Kushoto ni Mkuu wa Miradi Milele zanzibar Fourndation Bi khadija Shariff na kulia ni Bi Marie Louise Publlisher, Oxford University Press.
Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation imetoa vitabu laki mbili (200,000) vipya vya somo la Kiengereza kwa Skuli za Zanzibar na kushajihisha wanafunzi na watanzania kwa ujumla kuwa na tabia ya kujisomea.
Khadija Shariff, Mkuu wa Miradi, Milele Zanzibar Foundation aliyaeleza hayo wakati wa Uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili kwa waalimu ambao watafundisha wanafunzi wa sikuli za Zanzibar kwa kutumia vitabu hivyo.
Alieleza kuwa Vitabu vijulikanavyo kwa jina la “Let's Learn” English for Zanzibar Primary Schools" kwa darasa la 1-4 vilichapishwa na Shirika la Oxford University Press na kutathminiwa na kamati maalum ilikusanya wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).
“Uchapishwaji wa vitabu hivi ni sehemu ya matakwa na hamu kubwa ya Milele Zanzibar Foundation katika kuboresha utoaji wa elimu bora Zanzibar” alieelza Bi Khadija
Alieleza kuwa umakini na uangalifu mkubwa ulichukuliwa katika kufanikisha uchapishaji wa vitabu vyenye ubora wa juu kutokana na umuhimu mkubwa wa kuwatayarisha wanafunzi ipaswavyo kuweza kusoma, kuandika na kuzungumza kiengereza wakati watapofikia darasa la tano (5).
“Walimu nao wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuwa na vifaa na mbinu bora za kufundisha somo la kiengereza pamoja na kukuza uwezo wao wa kuongea lugha ya kiengereza” alieleza Khadija Shariff, Mkuu wa Miradi, Milele Zanzibar Foundation.
Vitabu vimefuata mtaala wa elimu ya msingi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na kulenga watoto wa kizanzibari kwa kuzingatia mila, utamaduni, historia na mazingira katika kubuni michoro na maudhui ya vitabu vya kiada.
Sambamba na kufuata mtaala mpya wa somo la kiengereza wa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa walimu wanauwezo wa kuwaandaa wanafunzi ipasavyo ili kufikia malengo ya kujifunza kama yalivyo ainishwa katika mtaala wa Taifa.
Mufululizo huo umejikita katika mbinu za mawasiliano na maudhui ili kujenga uwezo na ujuzi wa kusoma, kuandika, kuongea na kusikiliza na kutumika katika mazingira ya kila siku kupitia michezo, kufanya kazi kwa vikundi na michezo mingineyo.
Bi Fat-hiya Breik, mwalimu wa Kiengereza na English Resource Teacher wa Teacher Center ya Kiembe samaki, alisema kuwa , Mafunzo ya vitendo yaliomo katika kitabu yanawafanya wanafunzi wawasiliane na washiriki vizuri wakati wa masomo na pia inawasaidia kuwa wajasiri na kujiamini.
Alieleza kwamba muongozo umepitiwa ndani ya wiki hii ya mafunzo na kuwatayarisha walimu wa kiengereza wa Zanzibar kuwa na ujuzi unaotakiwa wa kufundisha vitabu na kuonyesha mbinu mbalimbali za kufundisha somo la kiengereza zinazowataka walimu kuwa imara katika kufundisha na kuwashirikisha wanafunzi kwa kutumia nyenzo, na kuboresha uelewa wa walimu na utumiaji wa lugha ya kiengereza.
“Tunafuraha kubwa si ya kuchapisha vitabu vya wanafunzi tu bali pia vitabu elekezi vya walimu vinavyoonyesha muongozo hatua kwa hatua katika utekelezaji wa kila somo kwa kutumia njia tofauti ili kufikia lengo lililokusudiwa ” alieleza Fatma Shangazi wa Oxford university Press.
Mafunzo haya pia ni fursa ya kujadili matatizo ya kawaida na changamoto zinazowakabili walimu wa kiengereza. "Let's Learn” English for Zanzibar Primary Schools” vitaanza kutumika madarasani Febuari 2017.
Milele Zanzibar Foundation inafanya tukio hilo ikiwa ni miongoni mwa utekelzaji wake wa dira ya kujenga na kuendeleza jamii ilio bora na imara Zanzibar.
Malengo ya Milele Zanzibar Foundation ni kuengeza kasi ya maendeleo katika maeneo ya afya, elimu na fursa za uchumi jamii katika vijiji na maeneo ya mbali kupitia miradi ya maendeleo yenye ukamilifu na endelevu
No comments:
Post a Comment