Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, baada ya kuunda timu mpya ya kusimamia ujenzi huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi. (Picha na Francis Dande).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitembelea Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, baada ya kuunda timu mpya ya kusimamia ujenzi huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi na kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi, Ray Mciob.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari, (hawapo pichani), mara baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la tatu la
Abiria (TB III), jijini Dar es Salaam. Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa
timu aliyoiteua kusimamia ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), mara
baada ya kuteuliwa leo jijini Dar es Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameteua timu mpya ya wataalamu saba
kwa ajili ya kusimamia mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal
III), katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Hatua hiyo
imefikiwa kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais John Magufuli alilolitoa jana
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza uwanjani hapo kujionea maendeleo yaliyofikiwa katika mradi
huo.
Timu hiyo inaongozwa
na Eng. Julius Ndyamukama inaundwa na Eng, Godson Ngomuo, Eng. Humphrey Kanyenye,
Eng. Abednego Lyanga, Eng. Mbila Mdemu na Eng. Rehema Myeya.
“Naamini timu
hii ina wataalamu mahiri, hivyo itasimamia ujenzi huu kukamilika kwa wakati na
kwa kuzingatia thamani ya fedha (value for money”, amesema Waziri Mbarawa.
Profesa Mbarawa
amemhakikishia mkandarasi wa kampuni ya BAM kutoka uholanzi inayojenga jengo
hilo kuwa Serikali itamlipa mkandarasi huyo katika kipindi cha wiki mbili
kutoka sasa.
Aidha, ameitaka
timu hiyo kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika mwezi Desemba mwaka huu
kama ilivyopangwa.
Kwa upande wake
Meneja wa mradi huo Eng. Julius Ndyamukama, ameahidi kushirikiana na wenzake
katika kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati.
Kiasi cha Shilingi
Bilioni 560 zinatarajiwa kutumika katika kugharamia ujenzi huo kwa awamu zote
mbili.
Katika hatua
nyingine Profesa Mbarawa amemsimamisha kazi Meneja wa Fedha kutoka Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege nchini (TAA) Bw. Simba Lugando kwa kuidhinisha malipo ya ujenzi
wa Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya kwa mkandarasi wa Kampuni ya DB
Shapriea kiasi cha shilingi Bilioni 3.3 ambapo ujenzi wake haukufanyika
ipasavyo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment