HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2017

Maalim Seif; Madai ya Prof. Lipumba ya kutokupokea simu yake si ya kweli


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungia mkono wanachama wa chama hicho waliompokea leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Bumbwini Misufini Kaskazini B Unguja akiwa katika ziara ya kuimarisha chama. (Picha na Talib Ussi). 


Na Talib Ussi, Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad ameeleza kuwa madai yaliotolewa na Prof. Ibrahim Lipumba kuwa hapokei simu zake hayana ukweli wowote.


Alisema kukumbuka zake zinamuonyesha kuwa  Prof. Lipumba alimpigia simu mara moja na alipoikuta alimpigia Lipumba lakini hakuipokea.


Aliayeleza hayo huko Bumbwini Misufufini  leo alipokua akiendelea na ziara yake ya kichama kwa upande wa kisiwa cha Unguja ambapo leo ametembelea ofisi za CUF zilizopo Wilaya za Kaskazini A na B.



"Ninachoweza kusema ni kuwa Profesa Lipumba alinipigia mara moja, na nilipoona simu yake mimi nikampigia lakini hakuipokea, Pia siku ya pili asubuhi nilimpigia tena simu na ikaita lakini hakuipokea" aliongeza.

Hata hivyo alieleza kuwa haoni haja ya kuwa na mazungumzo na Pr. Lipumba kwa kile alichadfai kuwa sio mwanachama tena wa chama hicho.

"Profesa Lipumba anadai tukakutane ili tukapange mikakati ya kukijenga chama, yeye si mwanachamwa wa Cu tukakutane kuzungumza nini?" alihoji.

Pia amesema watafuata taratibu za kisheria ili kuhakikisha chama hicho kinamaliza moja kwa moja mgogoro huo na kuwataka wanachama hao kuwa watulivu.


Akizungumza na wanachama wa chama hicho wa wilaya hizo, Katibu Mkuu huyo pamoja na mambo mengine aliwataka wanachama hao kushirikiana pamoja na viongozi wakuu wa CUF taifa wanaotambuliwa na baraza kuu la uongozi katika kukijenga na kukiimarisha chama hicho.


“Kuweni pamoja viongozi wenu waliohalali sio wale waliopandikizwa na msajili kwa matakwa ya CCM” alieelza katibu Mkuu huyo.



Akizungumzia hatua zilizofikiwa na Chama Cha CUF katika kudai kile kinachoitwa haki ya Wazanzibari, Maalim Seif amewataka wanachama hao kuwa watulivu na kuwahakikishia kuwa siku chache zijazo haki yao itapatikana.

"Nawahakikishia, tumepigana vya kutosha katika kuidai haki yenu na tumefikia hatua nzuri za kuweza kupata haki yenu" alisema.

Katika hatua nyengine, Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad aligusia mgogoro wa uongozi wa chama cha CUF uliotokana na hatua ya  Profesa Lipumba kuamua kurudi katika nafasi ya uwenyekiti wa chama hicho, na kusema watahakikisha wanapata ushindi.


Mapema Wanachama wa chama cha wananchi CUF walimueleza Maalim Seif kuwa  wako tayari kujitolea kwa hali na mali ili chama chao kiweze kufanyakazi zake bila hata kutetereka.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa chama hicho Wilaya ya kaskazini B katibu wa wilaya hiyo Khamis Abassi alimueleza katibu  kuwa wao wako tayari walale na njaa lakini chama kiweze kufanyakazi yake.

“Muache Msajili azuie Ruzuku, sisi tutakiharamia chama chetu mpaka pale tutakafikia malengo yetu” alieleza Abassi.

Alisema kwa sasa wameamua kutoa michango yao ya hali mali ili shighuli za chama hicho zizidi na kuimarika kwake na imani kwa Tanzania iongezeke maradufu.


Maalim seif yumon katika ziara ya kichama kwa mikoa yote ya zanzibar ambapo itaendelea hadi kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

Pages