Mratibu wa tamasha la Majimaji Selebuka, Reinafrida Rwezaura (kulia), akimkabidhi tiketi tatu za ndege jana, mmoja wa washindi wa mbio za baiskeli 2016, Allen Nyangiywa kwa ajili kushiriki mashindano ya baiskeli ya Afrika yanayojulikana kama Dis-Chem Ride For Sight 2017, yatakayofakanyika Afrika Kusini. (Picha na Francis Dande).
Na Lilian Lundo–MAELEZO
Washiriki watatu wa Tamasha la Majimaji Selebuka lililofanyika mkoani Ruvuma wanatarajia kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli nchini Afrika Kusini Februari 19, 2017.
Hayo yamebainishwa leo na Muandaaji Mkuu wa Majimaji Selebuka Reinafrida Rwezaura wakati wa makabidhiano ya tiketi za ndege za kwenda Afrika Kusini kwa washindi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAEELEZO jijini Dar es Salaam.
“Kikubwa kilichotukutanisha hapa leo ni kuwaaga washindi wa Mbio za Baiskeli katika tamasha la Majimaji Selebuka 2016, zilizofanyika tarehe 04 Juni 2016 kutoka Mbinga hadi Songea umbali wa kilomita 100, ambao wanatakiwa kwenda kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli Jijini, Johanesburg, Afrika Kusini,” alifafanua Rwezaura.
Rwezaura aliwataja washindi hao wanaotegemea kwenda Afrika Kusini kuwa ni Salum Miraji ambaye alikuwa mshindi wa kwanza , Allen Nyanginywa ambaye alikuwa mshindi wa pili na Ipyana Mbogela ambaye alikuwa mshindi wa tatu.
Kwa upande wake, mshiriki wa mashindano hayo Allen Nyanginywa ameishukuru Taasisi ya Songea Mississippi (SO-MI) kwa kuandaa mashindano hayo pamoja na kutimiza ahadi ya kuwasafirisha washindi wa kwanza hadi wa tatu kwenda nchini Afrika Kusini.
Aliendelea kwa kusema kuwa watahakikisha wanachukua ushindi nchini Afrika Kusini kwani huko wanaenda kufanya kazi na wamefanya mashindano hayo ya Baiskeli imekuwa ni kazi yao.
Majimaji Selebuka ni tamasha linalofanyika kila mwaka mjini Songea, mkoani Ruvuma ambalo huandaliwa na Taasisi ya Songea Mississippi (SO-Mi) ambapo kwa mwaka huu 2017 tamasha hilo linatarajia kufanyika kunzia Julai 23 hadi 30, 2017.
No comments:
Post a Comment