HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2017

TCCIA KUPELEKA WAFANYABIASHARA UTURUKI NA ITALY

Makamu wa Rais wa TCCIA Viwanda Octavian Mshiu akibadilishana nyaraka na Rais wa Chamber ya Biashara ya Uturuki 

Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) inatajia kufanya ziara ya Kibiashara Nchini Italy na Uturuki mapema mwezi Mei 2017.Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Ndugu Gotfrid Muganda alisema “ Lengo kubwa la ziara hii ni kuwawezesha wafanya biashara wa Tanzania kutanua wigo wa masoko na fursa za kibiashara na kubadilishana ujuzi“. Pia tukiwa Uturuki tunatazamia kusaini mkataba wa ushirikiano na chemba ya biashara ya Uturuki hii inafuatia ziara ya Rais wa Uturuki Nchini Tanzania.
Akizungumza juu ya ziara hiyo Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa Biashara na Masoko wa TCCIA Imani Kajula alisema “ Ukuzaji wa masoko ya nje ni mkakati endelevu ambao sio tu utaongeza soko nje lakini pia kuleta urari mzuri wa biashara na hivyo kusaidia kuimarisha pia thamani ya shilingi”. Aliwaambia wafanya biashara ambao ni wanachama na wasio wanachama wanakaribishwa kujiandikisha kuanzia sasa hadi tarehe 3 March 2017. Kwa taarifa zaidi info@eagroup.co.tz au muganda@tccia.com

No comments:

Post a Comment

Pages