Na Talib Ussi, Zanzibar
Maafisa 15 wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharbi Unguja wanatuhumiwa na kushiriki katika biashara ya dawa za kulevya Visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa mkoa hua Ayoub Muhammed Mahmoud wakati akizungumza na waandishi wa Habari Visiwani hapa.
Alileza kuwa kwa sasa watuhumiwa hao wa kijeshi wanashuhulikiwa kulingana na vyeo vyao, tayari kamishna wa Jeshi hilo Zanzibar amepokea majina ya watuhumiwa hao kwa ajili ya hatua zaidi.
“Hatujawakamata bado, ila kunataratibu za kejeshi ndio tunazoendelea nazo zikishakamilika hatua nyengine zitafuata” alieleza RC Mahmoud.
Sambamba na hilo Rc huyo alifahamisha kuwa kinyume na watuhumiwa hao pia wamekamata na kuwahoji waingiza na wauzaji nane (8) na wasambazaaji 24 ambao bado wanahojiwa.
Aidha lifahamisha kuwa wameyakamata maduka makubwa 16 ya wauza Madawa katika mkoa wake na kufahamisha kuwa kazi hiyo inaendelea.
Alieleza kuwa kwa staili yake hataji majina hasa baada ya ushauri wa kisheria mpaka muda utakapofika atafanya hivyo.
“Mwezangu Dar Salaam anastaili yake ya kutaja majina na mimi nnastaili yangu ya kimyakimya, mpaka ni hakikishe nimewamaliza ndio nitawaweka hadharani” alieleza Mkuu wa mkoa huyo ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa mjini Magharbi.
Alieleza kuwa asionekana kuwa hataji majina akaonekana anaogopa wauzaji hao , alidai hiyo ni mipango yake katika kupambana na waharamia hao.
“Siogopi kurugwa, sitishiki wala sibabaishwi katika kulinda heshimaa ya Nchi yangu pamaja na ndugu zangu kutokana madhara ya madawa haya” alieleza Mahmoud.
Alieleza kuwa anafanya kazi hiyo kwa niaba ya kuvikoa vizazi na kueleza kuwa hana nia ya kumuonea mtu wala kumdhalilisha.
Alisema kuwa afikia hatua ya kutotoa majina hadharani baada ya kupata ushauri na mbinu za kisheria kutoka wanasheria waliobobea.
“Hatuwezi kupigana kwa silaha moja kila mmoja atatumia silaha yake na mbinu zake lakini vita ni ile ile ya kuhakikisha tunatokomeza madawa ya kulevya” alieleza.
Alieleza muda ukifika wakiweka watu bayana hatojali cheo wala uwezo wake alionao katika nchi.
Alieleza kuwa Changamoto kubwa ambayo inawapa shida kukabiliana na madawa hayo ni kukosa vifaa vya kisasa katika bandari mbali mbali Visiwani humu vya kubaini madawa mara wahusika wanapoingia nchini.
Alisema kuwa wafanyabishara hao wana mbinu nyingi hasa kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha fedha kwa kile alichodai wanaweza kuhonga mtu yeyote na kiasi chochote.
“Kwa kushirikiana na maofisa walipo uwanja wa Ndege Zanzibar wafanyabiashara hawa wa madawa walimuuwa mbwa wetu tena ambaye alikua ni mtaalamu wa madawa” alileza.
Alieleza kuwa Nguvu kazi nyingi zimepotea na maadili yameshuka na pia udhalilishaji na wizi umeongezeka kutokana na utumiaji wa madawa hayo.
“Katika kukabiliana tumeandaa mpango wa kuleta vifaa ambavyo vitaweza kuichaguza ndege mzimaa na hata kontena ndani ya meli” alieleza Rc huyo.
No comments:
Post a Comment