HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2017

AFRICA JOB CENTER KUWANUFAISHA WATANZANIA KATIKA KUPATA AJIRA


Msemaji wa Kampuni ya Africa Job Center, Doris Godfrey, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kupitia kampuni hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Idara ya Mauzo, Edgar Soka.
 Msemaji wa Kampuni ya Africa Job Center, Doris Godfrey, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kupitia kampuni hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Idara ya Mauzo, Edgar Soka.
Ufafanuzi.

Na Mwandishi Wetu

VIJANA wametakiwa kutumia simu zao za mkononi kwa manufaa zaidi ikiwa ni pamoja na kujitafutia ajira kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi, Msemaji wa Kampuni ya Africa Job Center (AJC), Doris Godfrey, ambayo inawasaidia watu mbalimbali kupata kazi barani Afrika alisema teknolojia imerahisisha vitu hivyo ni rahisi kufuatilia na kujua kinachoendelea.

Alisema  wameamua kuwa kampuni ya vijana wa kitanzania ambao wanakazi ya kuwaunganisha wanaotafuta ajira na waajiri kutoka nchi tofauti ikiwa ni pamoja na Kenya, Burundi, Malawi na Rwanda.

“ Mtu anaweza kupata kazi  kwa kupitia mtandao na simu yake ya mkononi kwani unaweza kuwasiliana na muajiri moja kwa moja kupitia tuvuti yetu nakujipatia ajira”. alisema.
Alisema nafasi za kazi zilizopo katika tovuti yao ni kwanzia ngazi ya chini kabisa ya kufagia paka ngazi ya juu, ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wanaweza kutoa matangazo yao.

Pia alisema kutakuwa na matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu wasio na ajira kutambua kuwa wanaweza kupata ajira nje ya Tanzania. www.africajobcenter.com

No comments:

Post a Comment

Pages