Mwenyekiti wa Chama Cha Wakandarasi Tanzania, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki akisistiza jambo kwa waandishi wahabari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam kuhusu Serikali kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani katika miradi ya ujenzi.
Na Eliphace Marwa, Dar es salaam
Chama
cha Wakandarasi Tanzania kimeiomba Serikali kuwashirikisha katika zabuni za
ujenzi wa miradi mbalimbali ya umma Wakandarasi wazawa.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti
wa Chama hicho, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki wakati mkutano na waandishi wa
habari kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Alisema
kuwa wanaiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuwashirikisha wakandarasi wa
kitanzania , wakimemo wakandarasi wa madaraja yote ili waweze kujijengea
kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa
majengo mbalimbali ya Serikali mkoani Dodoma.
Mhandisi
Mwakyambiki aliongeza kua hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira kwa vijana na
Kampuni za kitanzania katika shughuli za ujenzi hapa nchini.
Aidha,
Chama hiyo kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa mstari wa mbele
katika kutekeleza mikakati na kusimamia sekta ya ujenzi hapa nchini.
Aidha
Mwakyambiki aliongeza kuwa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano
kuhamia Dodoma ni vema wakandarasi wa ndani wakapewa fursa ya kushiriki katika
kandarasi mbalimbali ambazo serikali inatarajia kuzifanya huko Dodoma.
Kwa
upande Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi John Bura alimshukuru
Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuitikia wito wa wakandarasi kwa kuwatengea
miradi michache ambayo ilikwisha tangazwa.
Aliwataka
wakandarasi kuunda umoja kwa ajili ya kuitekeleza kwa weledi ili kuongeza imani
kwa Serikali.
No comments:
Post a Comment