Na Jovina Bujulu, Dar es salaam
Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi inatarajia kuendesha kongamano la siku moja kwa vijana wanaosoma mafunzo ya fani ya ugavi katika vyuo mbalimbali nchini, tarehe 25, Machi mwaka huu, jijini Dra es Salaam.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo wa Bodi hiyo Ndugu Amani Ngonyani wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
“Lengo la kongamano hilo ambalo ni la kwanza ni kuwabadilisha vijana hao kimawazo, mwelekeo na maono kuhusu kujiajiri hususani katika fani hiyo,’ alisema ndugu Ngonyani.
Aidha kongamano hilo litawawezesha vijana kutumia fursa zilizopo na kuona namna gani wanaweza kujiajiri kwa kuunda vikundi ili kuweza kupa mikopo na ufadhili kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kuwa kongamano hilo litatanguliwa na mafunzo ya siku moja yatakayofanyika tarehe 25, Februari mwaka huu na kuwashirikisha viongozi wote wa jumuiya ya wanafunzi wa ununuzi na ugavi.
“Lengo la mafunzo hayo ni kuwajenga kimaadili viongozi hao na kuwaandaakulitumikia Taifa kwa uzalendo pindi wamalizapo masomo yao, ili kuchochea uchumi wa viwanda,” aliongeza Ndugu Ngonyani.
Mada kuu katika kongamano itakuwa ni “mchango wa fani ya ununuzi na ugani katika kukuza na kuendeleza viwanda”. Aidha mada nyingine tofauti zitakazowasilishwa ili kuwajengea vijana uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
No comments:
Post a Comment