Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameteua Kamati Maalum
ya Hamasa kuelekea Mashindano ya AFCON chini ya umri wa miaka 17
yatakayofanyika mwezi May 2017 nchini Gabon ambapo Tanzania inawakilishwa na
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana (Serengeti Boys).
Kamati
hiyo ya watu kumi(10) itaongozwa na Mwenyekiti Charles Hillary kutoka Azam Tv na
Katibu wake Selestine Mwesigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa kamati hiyo ni Dkt Hassan Abass Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ruge Mutahaba Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group.
Wengine ni Hoyce Temu Mrembo wa
Tanzania mwaka 1999, Maulid Kitenge Mtangazaji kutoka EFM, Beatrice Singano
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Erick Shigongo Mkurugenzi wa Global
Publishers na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba na Naseeb Abdul
(Diamond Platinumz).
Lengo kuu
la Kamati hii ni kuhamasisha watanzania kuiunga mkono Timu ya Serengeti Boys na
juhudi za Serikali katika kuhakikisha wanarudi na ushindi katika mashindano
hayo.
Imetolewa na
Zawadi Msalla
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
28/02/2017
No comments:
Post a Comment