HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

May 16, 2017

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA 22 WA WANAHISA JIJINI ARUSHA MEI 20

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuelezea Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika Mei 20 jijini Arusha.  Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki hiyo, Esther Kitoka. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuelezea Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika Mei 20 jijini Arusha.  Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki hiyo, Esther Kitoka na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay.  

 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akifuatilia mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akifuatilia mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.

NA GLORY CHACKY

WANAHISA wa Benki ya CRDB wametakiwa kushiriki katika Mkutano Mkuu utakaofanyika Arusha ili kupata uelewa zaidi juu ya hisa.

Mkutano huo wa 22 toka kuanzishwa kwa benki hiyo, unaotarajiwa kufanyika Mei 20 mwaka huu ambapo wanahisa watapata kufahamu fursa na changamoto za uwekezaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, katika mkutano Mkuu wa wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dk. Charles Kimei alisema katika mkutano huo watajadili mambo mbalimbali ya kampuni.

"Mkutano huo utaambatana na semina maalumu kwa wanshisa juu ya fursa mbalimbali za masuala ya uchumi, fedha na uwekezaji"alisema.

Alisema kutokana na mabenki kuwa na changamoto nying ni wakati wa wanahisa kujua benki yao inafanya nini kwasababu wanahisa wengi hawana uelewa.

No comments:

Post a Comment

Pages