Mwenyekiti wa Sekretarieti ya
Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni
Mgeni Rasmi, Adatus Magere akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya kuzuia
biashara hiyo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa,
Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika nchi
zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo
yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu. Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya kupambana na biashara hiyo, ambaye pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso . Mafunzo yanashirikisha wajumbe kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Binaadamu, Separatus Fella, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu yanayoshirikisha nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada kutoka nchini Zimbabwe, Jacinta Hofnie, akiwasilisha mada kwa washiriki wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere (watatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
Hali ngumu ya maisha ikiwepo ukosefu wa
mahitaji muhimu imetajwa kama sababu kubwa inayochochea Biashara Haramu ya
Usafirishaji wa Binadamu huku waaathirika wa biashara hiyo wakiahidiwa maisha
mazuri katika nchi wanazopelekwa.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo
ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Mwenyekiti
wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa
Binadamu (ATP), ambaye pia ni mgeni rasmi katika mafunzo hayo, Adatus
Magere amesema wahusika wa biashara hiyo
wamekua wakiwarubuni waathirika wa biashara hiyo kuwapatia maisha mazuri na kujikuta wakiingia katika
madhara ya biashara hiyo.
Aliongeza kuwa kuna umuhimu
kwa watunga sheria na vyombo vya sheria kutunga sheria zitakazo saidia
kutokomeza kabisa biashara hiyo kwani imekua ikiendelea kukua siku hadi siku
hali inayopelekea idadi ya wahanga wa biashara hiyo kuendelea kuongezeka.
“Tunaomba watunga sheria na wasimamiaji wa
sheria kusaidiana kwa pamoja katika kudhibiti na kuzuia biashara hiyo kwa kutoa
adhabu kali kwa wale watakaobainika kuhusika moja kwa moja na biashara hiyo ili
tatizo hili liweze kuisha katika nchi zetu,” alisema Magere.
Aidha Katibu Mkuu wa Sekritarieti ya
Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu ambaye pia ni
mwenyeji kwenye mafunzo hayo, Seperatusi Fella, amesema kuwa ili kuweza
kupambana na kuzuia biashara hiyo kuna umuhimu kwa wadau mbaimbali kutoa elimu
na mafunzo juu ya athari zitokanazo na usafirishaji haramu wa binadamu, hivyo
mafunzo ya mara kwa mara ni muhimu kwa wananchi na wadau mbalimbali.
Naye Mratibu wa mradi wa Shirika la Wahamiaji
la Kimataifa (IOM), Tamara Keating ameahidi kushirikiana na mashirika mbalimbali
ili kukomesha biashara hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ili kupata taarifa ya wahusika wa biashara hiyo.
Ripoti na tafiti mbalimbali za kimataifa
juu ya biashara hiyo zinaonesha Tanzania ni mojawapo kati ya nchi nyingi
zinazohuishwa na biashara haramu ya usafirishaji binaadamu ambapo waathirika
wengi wa biashara hii ni watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoahidiwa kazi nzuri
na maisha mazuri pindi wafikapo katika nchi wanazopelekwa.
Mafunzo
hayo yanafanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam
yakiwa na lengo la kuleta uelewa wa jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa pamoja na
kuleta ushirikiano katika kukomesha biashara haramu ya usafirishaji binadamu
baina ya wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment