HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 11, 2017

LAPF YADHIHIRISHA KUWA CHAGUO BORA KWA WAAJIRIWA WAPYA


 Meneja Masoko na Mawasiliano Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo mjini Dodoma leo. Kushoto ni meneja Matekelezo wa LAPF Victor Kikoti.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari Mjini Dodoma walioshiriki katika mkutano wa LAPF Dodoma leo. LAPF imedhihirisha kuwa Chaguo Bora kwa Waajiriwa wapya.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mfuko wa Pensheni wa LAPF umekuwa ni chaguo la wanachama hasa waajiriwa wapya kutokana na ubora wa huduma zinazotolewa pamoja na kutekeleza ahadi zake kwa wanachama. Hivi karibuni Serikali ilitoa ajira za walimu wa sayansi 3,084. 

Katika walimu hao walioripoti katika vituo vyao vya kazi walikuwa walimu 2,792 na katika hao walioripoti LAPF iliibuka kidedea baada ya walimu 1,888 kuchagua kujiunga na LAPF sawa na asilimia 68 ya walimu wote walioripoti.

Hii inadhihirisha wazi kuwa Mfuko wa LAPF ndio Mfuko bora wa Pensheni hapa Tanzania. LAPF imekuwa na ongezeko kubwa sana la wanachama kutoka sekta binafsi na serikalini kutokana na huduma zinazotolewa ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama wake na haswa waajiriwa wapya.

 Hadi kufikia mwezi Aprili 2017, Mfuko wa LAPF una wanachama zaidi ya 172,000 ambapo ndani ya mwaka wa fedha 2016/2017 pekee LAPF imeandikisha wanachama wa kisheria 16,839 na wa Hiari kupitia LAPF Jiongeze Scheme 645. 

Baadhi ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF ni pamoja na Mikopo ya kujikimu kwa waajiriwa wapya ili waweze kujikimu na mahitaji muhimu mara wanapoanza ajira  ambapo hadi sasa wanachama 518 wamenufaika na mkopo huu maarufu kama Maisha Popote na LAPF. 

Kadhalika pia LAPF inatoa mikopo ya elimu kwa wanachama wake kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.  Hadi sasa LAPF imeweza kutoa mikopo hii kwa wanachama 1438 yenye thamani ya shilingi 2.4 bilioni. 

LAPF pia inatoa mafao ya uzazi kwa wanachama wake ambapo wanachama wanawake wanapojifungua hulipwa asilimia 129.3% ya mshahara wao kama mafao ya uzazi. Hadi sasa tangu kuanzishwa kwa fao hili wanachama 11,744 wamelipwa mafao uzazi yenye thamani ya shilingi bilioni 9.54. 

LAPF ndio Mfuko pekee hapa nchini ambao unaowalipa wanachama wake mapema na hata siku chache kabla ya kustaafu. Tangu kuanza kwa utaratibu huu wanachama 1691 wamelipwa  mapema kabla ya tarehe ya kustaafu. 
Takwimu hizi zinadhihirisha wazi utekelezaji wa ahadi kwa wanachama wa LAPF. 

ISHI NA KUSTAAFU KWA UFAHARI NA LAPF

No comments:

Post a Comment

Pages