HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 08, 2017

SMZ YATUMA SALAMA ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono  wa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo kutokana na vifo vya Wafanuzi 32, Walimu pamoja na Dereva  wa Skuli ya Mchepuo wa Kingereza ya Luck Vicent kufuatia  Basi walilokuwa wakisafiria kupindika katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Salamu hizo za pole zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (pichani), kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Wananchi wote wa Zanzibarn kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa.

Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wa Zanzibar wamepokea kwa huzuni, masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Rhotia, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha na kusababisha  vifo hivyo pamoja na Majeruhi kadhaa.

Alisema huo ni msiba mkubwa siyo tu kwa Wazazi, Ndugu na Jamaa wa Watoto hao bali pia ni kwa Taifa zima, kwani Watoto hao walikuwa nguvu kazi kubwa iliyotumainiwa kuja kulitumikia Taifa laWatanzania baada ya kumaliza Masomo yao.
Balozi Seif  alimuomba Mwenyezi Mungu awape wazazi na familia za Watoto hao moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hichi kigumu cha msiba na Wananchi wote Nchini Tanzania wako pamoja katika msiba huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia alimuomba Mwenyezi Muungu mola wa viumbe wote azilaze roho za marehemu wote mahali pema pepono amin na wale majeruhi awaponyeshe haraka ili warudi kuendelea na maisha yao ya kila siku.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
7/5/2017.

No comments:

Post a Comment

Pages