Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, akizungumza baada ya kutangaza kujiuzuru Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika jijini Arusha leo. (Picha na Francis Dande).
Wanahisa wakiwa katika katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika jijini Arusha.
Na Francis Dande, Arusha
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, ametangaza kujiuzuru Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kutokana na kubanwa na majukumu mengi ya kijamii pamoja na ya kisiasa.
Sumaye alitangaza uamuzi huo katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
"najizuru kutokana na kubanwa na shughuli nyingi ambazo zinanibana kwa sasa. naomba nimpishe mtu mwingine ambaye ataendeleza mafanikio ya benki hii," alisema.
sumaye anahudhuria mkutano mkuu huo ambao umetangaza kutoa gawio la Shilingi kumi kwa kila hisa moja kwa wanahisa wake mwaka huu.
Kufafanua juu ya uamuazi wake, sumaye alisema anafanya hivyo ili benki hiyo isihusishwe na msimamo wake wa kisiasa na kuingilia utendaji wake kwa namna moja au nyingine.
alisema kutokana na mgongano wa maslahi uliopo, kwa ridhaa yake, bila kushinikizwa na mtu yeyote, ameamua kuachia wadhifa huo ili kupata muda wa kutosha kushughulikia masuala yake binafsi pamoja na kuimarisha chama chake kipya.
"Naomba mtu mwingine achukue nafasi hii. Mimi nitaendelea kuwa mwanahisa wa kawaida wa benki yetu. sitaki mambo yangu yaingiliea ufanisi wa benki yetu," alisema Sumaye.
No comments:
Post a Comment