Mkuu wa Kitengo cha Fedha Tigo Pesa, Christopher Kimaro, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kampuni hiyo kuwalipa wateja wake gawio la robo mwaka la Shs. bilioni 63.58 kama faida ya gawio lao tangu kuanza kwa mpango huo mwaka 2014. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Usambazaji, Catherine Rutenge. (Picha na Francis Dande).
NA MWANDISHI WETU
WATUMIAJI wa simu za mkononi wamepewa gawio la fedha ambapo
gawio hilo huwa linatolewa katika kila robo ya mwaka.
Hiyo ni mara ya 12 kwa watumiaji wa simu za mkononi kupewa gawio
la robo ya mwaka ambapo huduma hiyo ilianza kutolewa tangu mwaka 2014.
Akizungumza Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha
Tigopesa, Christopher Kimaro, alisema kuwa wamekuwa wakitoa gawio hiyo kama
faida kwa watumiaji wote wa simu za mkononi.
Alisema kuwa malipo hayo ni faida inayopatikana katika akaunti
za mfuko ambazo zipo katika benki mbalimbali za kibiashara nchini.
Alisema kuwa waliopokea gawio hilo ni watumiaji wa simu za
mkononi, mawakala wa rejareja, mawakala wakubwa na washirika mbalimbali wa
kibiashara kulingana na kiasi cha thamani ya fedha waliyonayo.
“Tumetoa gawio la faida kwa mara ya 12 mfululizo, hili lipo
katika mikakati yetu ya kujikita kutoa na kufikiwa kwa huduma za kifedha kwa
wateja wetu nchi nzima,” alisema Kimaro.
Alisema kwamba kuongezeka kwa faida katika huduma zao
kunaboresha mazingira ya soko na kukuza biashara za mbalimbali kwa watumiaji wa
simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment