Na Talib ussi, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza matumizi ya Makadirio ya Mapato kiasi cha Trilioni 1,081.4 mwaka wa fedha 2017-2018 ikitegemea makusanyo ya kodi za ndani na kuachana na washiriki wa maendeleo.
hayo yalielezwa na Waziri wa fedha na mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Dk. Khalid Salum Mohamed akitoa muelekeo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017-2018 alipozungumza na waandishi wa habari Visiwwani hapa.
Alieleza kuwa makadirio hayo ya makusanyo na matumizi hayatahusisha vyanzo kutoka nje na badala yake watatgemea vynzo vya ndani kwa kutimia makusanyo ya TRA na ZRB.
Alifahamisha kupitia TRA wanatarajia kukusanya jumla ya sh.Bilioni 258.7, na ZRB inatarajiwa kukusanya jumla ya sh.347.3 Bilioni.
No comments:
Post a Comment