HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2017

15 Waingia Fainali ya European Youth Film Compitition 2017

Balozi wa Umoja wa Ulaya, Roeland van de Geer, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa akitangaza washindi bora 15 waliongia katika shindano la uandaaji wa filamu ‘European Youth Film Compitition 2017’. (Picha na Francis Dande).

NA NEEMA MWAMPAMBA

UMOJA wa Ulaya kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa na Undersons Media wametangaza majina ya washindi 15 waliopita katika mchujo wa uandaaji filamu ‘European Youth Film Compitition’.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Balozi wa Ulaya hapa nchini Roelans Van de Geer, alisema washindi hao walipatikana kutoka kwa washiriki 35 waliopita katika mchujo wa awali.


Alisema washindi hao walipatikana kutokana na ubora wa Maudhui, ubunifu na ubora wa filamu walizokusanya, ambapo kila mmoja alitakiwa kubini stori na kuitengenezea filamu kisha kuwasilisha kwa waandaaji ambao waliweza kuzipitia na kutoa maksi zilizopelekea kupata washindi hao.


Akitaja washindi hao Mratibu wa Undersons Media Mussa Sakara alisema kuwa ni Christine Pande, Cornel Mwakyanjala, Daniel Manege, Dennis Chacha, Dosi Said, Florence Mkinga, Francis Nyerere na Frank Machiya.
Wengine ni Freddy Freddy Feruzi, Karim Michuzi, Kherry Kafuku, Louis Shoo, Malik Hamis, Rashid Songoro, Taragwa Marwa na Wambura Mwikabe.


Alisema mara baada ya washindi hao kupatikana hatua inayofuata ni kupeleka filamu zao kwa watazamaji ambao wataweza kupiga kura na kuchagua filamu waliyoipenda kati ya zilizoshinda.


“Kuna kipengele cha Viwers Choice Award, ambacho watazamaji watasema filamu waliyoipenda na baada ya hapo tutarudi kwa wataalamu ili kujua ipi ni bora kuliko nyingine kwa kuzingatia maudhui, ubora wa picha na vitu vingine muhimu” alisema Sakara.


Aidha alisema hatua itakayofuata ni kupata filamu zitakazoingia kwenye tano bora na baadaye kuwapata washindi watatu ambapo wa kwanza atapata zawadi yenye thamani ya Sh. milioni saba, wa pili Milioni tano na watatu atapata milioni tatu.


Akizungumzia shindano hilo Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Basata Wilhard Tairo alisema shindano hilo limekuja wakati mwafaka ambao tasnia hiyo inahitaji kubaini, kuibua na kuendeleza vipaji kwa ajili ya vizazi vijavyo.

No comments:

Post a Comment

Pages