Na
Agness Moshi na Jonas Kamaleki- MAELEZO
Zaidi
ya nusu ya Watanzania wamesema kuwa hali ya usalama nchini imeimarika ikilinganishwa na miaka takriban miwili
iliyopita na kuwafanya wananchi waishi kwa utulivu na amani.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali lijulikanalo
kama Twaweza, Bw. Aidan Eyakuze wakati akiwasilisha matokeo utafiti wa “Hapa Usalama
Tu: Usalama, Polisi na Haki nchini Tanzania” kupitia sauti za wananchi kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Bw.
Eyakuze alisema kuwa takwimu zilizo kusanywa na sauti za wananchi kwa mwaka huu
zimeonesha kuimarika kwa usalama kwa wananchi wa Tanzania Bara ikilinganishwa
na miaka iliyopita.
“Tumeongea
na watu 1805 kuwauliza hali ya usalama katika maeneo wanayoishi na asilimia 53
ambayo ni sawa na nusu ya Watanzania Bara wamesema hali ya usalama imeimarika
na inaridhisha” alisema Bw.Eyakuze.
Bw.Eyakuze
amesisitiza kuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa wananchi wenyewe, kupitia simu zao za mikononi ambapo wameona
kuwa watanzania wengi wapo kwenye hali ya usalama na hii inamewapa taswira
tofauti na taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari.
Aidha,
Bw.Eyakuze amesema kuwa asilimia 47 ya wananchi wanaridhishwa na utendaji kazi
wa jeshi la Polisi nchini kutokana na kuzuia na kutatua uhalifu na kuwajali
wananchi.
Ripoti
hiyo imeonyesha kuwa wananchi wanapata pia ulinzi kutoka kwa polisi jamii,
maarufu kama sungusungu na asilimia 41 ya wananchi wamesema wana vikundi vya
sungusungu katika maeneo yao na wanaridhika na huduma zinazotolewa.
Utafiti
huu ulifanyika mnamo Aprili 2017 ukihusisha mikoa yote ya Tanzania Bara na wa
kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumuia simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment