WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.
Ametoa kauli leo (Ijumaa, Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya
mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu
amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda
mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.
“Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria,
hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za
uchumi, afya, elimu na ulinzi.”
Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa
Tanzania katika kuimarisha miradi ya
maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Pia
Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India kuja kutembelea maeneo ya utalii nchini ukiwemo mlima wa Kilimanjaro, mbuga
za wanyama na visiwa vya Zanzibar.
Kwa
upande wake, Mkuu
wa Majeshi wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano
inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.
Amesema
wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika
mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan
maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA,
JULAI 28, 2017
No comments:
Post a Comment