NA KENNETH NGELESI,MBEYA
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt John Pombe Magufuri, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika Mkutano wa Mkuu Taifa
wa Jumuhiya ya Serikali ya Mitaa wa, ALAT, ambao kitaifa utafanyika Jijini
Mbeya, kuanzia Agosti 19 hadi 22, mwaka huu.
Mkutano huo ambao utafanyika katika Ukimbi wa
Mkapa,ni wa 33 na kwamba unatarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 800 wa ndani
ya nchi pamoja na wadau mbalimbali kutoka nje ya nchi.
Taarifa ya Mkutano huo ilitolewa jana kwa waandishi wa habari jijini hapa na , Makamu
Mwenyekiti ALAT Taifa, Stephen Mhapa baada ya kumaliza kutembelea na kukagua
eneo litakalofanyika mkutano huo.
Akizungumza na waandishi Mhapa alisema kuwa Mkutano
huo, unafanyika Mbeya kutokana na ombi maalum lililoombwa na Meya wa Jiji la
Mbeya, David Mwashilindi kwa kushirikiana na wenyeviti wa halmashauri kutokana
na changamoto za kimamlaka zinazozikabili halmashauri hizo katika utendaji
kazi.
Alisema mkutano huo ni fursa kwa wakazi wa jiji
la mbeya na halmaashuri waone ni nimna gani wanaweza kuzitumia ugeni unaeweza
kuwanufaiasha.
‘ALAT Kama
tunavyofahamu kazi kubwa ya ALAT ni kuhakikisha inatoa elimu kwa wajumbe wake
ili wafahamu mipaka ya madaraka na ya kiutendaji lengo likiwa ni kupunguza au
kutokomeza migogoro isiyo ya lazima inayozikumba halmashauri,”alisema.
Aidha, alisema kuwa mkutano huo, Rais Magufuli ataambana
na viongozi akiwemo waziri mwenye dhamani na wizara hiyo pamoja na katibu Mkuu
lakini pia pia utashirikisha nchi wanachama wa Jumuhiya ya Afrika Mashariki
kutoka nchi ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Akizungumzia Mkutano huo, Meya wa Jiji la
Mbeya, Mwashilindi, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya, kuhakikisha wanatumia
fursa hiyo katika kukuza uchumi pamoja na kutangaza bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa ndani ya eneo hilo.
“Tumepokea kwa mikono miwili jukumu la kuaandaa
mkutano huu, na sisi kama Jiji tupo vizuri na tunaendelea na maandalizi kwani
hata uongozi ALAT, Taifa wameridhika na mahali patakapo fanyika
Mkutano,”alisema.
Hata hivyo, alisema mkutano huo ni fursa kwa
wajumbe mbalimbali hasa Madiwani ili kufahamu namna ya uendeshaji wa
halmashauri na kufahamu mipaka ya majukumu yao ili kuepusha migogoro isiyo ya
lazima.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Alat Mkoa wa Mbeya
Mwalego Chisengo alisema kuwa Mkutano una manufaa kwa wananchi wa Mkoa Mbeya
hivyo ni fursa Pekee kwa wananchi kutumia.
‘Mkutano huu ni fursa kwa wananchi hasa katika
eneo la Uchumi hakuna asiye fahamu kuwa Mbeya tunazalisha vyakula hivyo uwepo
wa wageni ni fursa na wajibu wetu kuitumia kwani wageni hawa watakuja na fedha
tutauza vyakula lakini pia watalala kwenye nyumba zetu za kulala wageni’
alisema Chisengo
No comments:
Post a Comment