WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa maelekezo ya namna ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka sita, kati ya uongozi wa Kiwanda cha Saruji Mbeya na wananchi wa kijiji cha Nanyala, wilayani Mbozi.
Mgogoro
huo, umetokana na Kiwanda cha Saruji Mbeya, kupewa eneo la kijiji hicho
chenye ekari 2,315 na uongozi wa mkoa wa Mbeya bila ya makubaliano na
wanakijiji hali iliyosababisha wagome kuondoka.
Pia
Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa ya Songwe Luteni Mstaafu Chiku
Gallawa na wa Mbeya Bw. amos Makalla kukutana na kufanya mazungumzo ya
kulirudisha eneo hilo mkoa wa Songwe.
Waziri
Mkuu alitoa uamuzi huo leo (Jumatatu, Julai 24, 2017) baada ya wananchi wa
kijiji hicho kuzuia msafara wake kwa lengo la kumuelezea changamoto yao ya
kudhulumiwa ardhi yao na kukabidhiwa kwa muwekezaji bila ya kushirikishwa.
Amesema
Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ni sikivu
na inawajali wanyonge ndio maana amesimama ili aweze kusikiliza kero zao na
kuzipatia ufumbuzi, hivyo amewaomba waendelee
kuiamini na watarudishiwa ardhi yao.
Pia,
Waziri Mkuu ameiagiza Kampuni ya Saruji Mbeya kuondoa kesi iliyoifungua
mahakamani dhidi ya wananchi wa eneo hilo, ili waweze kukutana na Serikali
pamoja na wananchi hao kwa ajili ya kujadili namna bora ya uwekezaji katika
eneo hill.
Amesema
kiwanda hicho kilipewa eneo hilo la mkoa wa Songwe kimakosa na mkoa wa Mbeya kwa
ajili ya kupata malighafi ya kutengenezea saruji, amesema Serikali haiwazuii
kulitumia eneo hilo ila wakubaliane na wananchi kwanza.
“Hatuzuii
kiwanda kufanya kazi ila tunataka mkubaliane na wananchi kwanza ili kuondoa
migogoro. Wananchi wanahitaji viwanda ila si kwa migogoro. Wananchi nawaomba
muendelee kuwa na amani na hakuna atakayechukua ardhi yao bila ya ridhaa yao.”
Eneo
hilo lilikuwa mali ya Serikali toka mwaka 1987, ambapo wakati Kampuni ya Saruji
Mbeya ilikuwa inamilikiwa na Serikali, kabla ya kubinafsishwa.
Wananchi hao wamesema wamefurahishwa na uamuzi huo wa Waziri
Mkuu wa kutatua mgogoro huo ambapo wananchi hao walidai kwa muda mrefu ulikuwa ukiwasumbua
kwa kutakiwa kuondoka katika eneo lao bila na kukabidhiwa kwa muwekezaji bila ya
kushirikishwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe amemshukuru Waziri Mkuu kwa
kulitolea tamkoa suala hilo na kwamba atakutaka na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa
ajili ya utekelezaji wa agizo hili ili wananchi waweze kuishi kwa amani katika
ardhi yao.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU,
JULAI 24, 2017
No comments:
Post a Comment