Na Talib Ussi, Zanzibar
Jumuiya ya Vijana ya
Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) imeeleza kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana
limekuwa sugu na linasababisha athari kubwa kwa vijana waliowengi nchini
Tanzania kwa madai kuwa Serikali zoote mbiliu zimekosa mipango dhidi ya yao.
Kauli hiyo ilitolewa
jana na Mkurugenzi wa Habari wa Jumuiya ya Vijana chama hicho JUVICUF Abeid
Khamis Bakar kupitia taarifa kwa vyombo vya habari
Alifahamisha kwamba
tatizo ambalo limezidi kutokana na mwenendo wa serikali mpya chini ya
Rais John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kushindwa kuweka
mikakati ya kuwaajiri vijana na badala yake kuwanyanyasa wale ambao
wamejiajiri.
Alieleza kuwa
vijana wengi wamesambaa mitaani bila ya kazi ya kufanya licha ya kuwa na sifa
ya kuajiriwa lakini alidai kuwa Serikali hizo zinaonyesha hazina malengo mazuri
kwa vijana wa Nchii.
alifahamisha kuwa kwa
upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ( SMZ), tatizo ni kubwa zaidi,kwa
maelezo kuwa tangu kuingia madarakani kwa njia isiyokuwa ya kidemokrasia,
serikali ya Dk. Ali Muhammed Shein haijatangaza ajira toshelezi (hajafikia hata
thumni ya mahitaji ya ajira kwa vijana) pamoja na ukweli kwamba wapo vijana
wengi walioomba nafasi za kazi maeneo tofauti kama vile katika Benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) na hadi kufanya usaili miezi kadhaa lakini hakuna jibu lolooote
walilopewa hadi leo.
“Wanajigamba
wanaserikali lakini vijana wao hawana ajira hata hawashughuliki, tujiulizeni
walichaguliwa kweli na wananchi hawa” aliuliza mkurugenzi huyo wa habari
JUVICUF.
alisema kuwa wanapata
imani kuwa SMZ haina uwezo wa kutoa ajira kwa vijana hasa kwa kuzingatia kwa
madai kuwa hivi karibuni kulitangazwa nafasi za ajira katika Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege Zanzibar, na vijana zaidi 100 kutoka Unguja nan Pemba na
wakati nafasi zinazotakiwa ni mbili tu na hadi leo hakuitwa mtu.
“ Hii ina maana
mahitaji ya ajira ni makubwa zaidi ya uwezo wa serikali. Zanzibar kuna
malalamiko ya mwenendo usiofaa wa serikali na taasisi zake kutoa fursa za ajira
kwa upendeleo unaozingatia misingi ya kiitikadi (mirengo ya kisiasa). Hili ni
tatizo kubwa kama lilivyo la kuzuia fursa za kupanda daraja na kujiendeleza
kielimu kwa wafanyakazi waliopo serikalini” alieleza.
JUVICUF Taifa kwa
kuyaona hayo na mengine mengi, imewaomba vijana popote walipo katika nchi yao,
kutovunjika moyo kwa mwenendo wa mfumo unaowakwamisha katika fikra za
kimaendeleo.
Aidha imewataka
vijana wote nchini washikamane kwa kuwa kitu kimoja katika kukemea
uzuiaji wa haki zao unaofanywa na Serikali au kikundi chochote kile na
waendelee kuamini kuwa kufikiri na hatimaye kuamua kwa ajili ya maslahi yao ya
kimaendeleo, ni haki yao isiyonyang’anyika kwa mujibu wa katiba.
Alieleza kuwa inafaa
kukemewa kwa namna yoyote ile na inapotokea wanapaswa kushikamana na kuipigania
kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kikatiba zilizopo.
“Ndipo
watakapojihakikishia mustakbali wao kuhusu maendeleo ya kiuchumi, kielimu,
kisiasa na kiutamaduni” alieleza Bakar.
No comments:
Post a Comment