HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 27, 2017

SIMBA YAISHUSHIA KIPIGO CHA 7-0 RUVU SHOOTING

 Nyota wa mchezo kati ya Simba na Ruvu Shooting, Emmanuel Okwi (kushoto), akipongezana na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake moja kati ya mabao 4 aliyofunga katika mchezo wa fungua dimba la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting. (Picha na Francis Dande).
  Wachezaji wa Ruvu Shooting wakijadiliana jambo baada ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (hayupo pichani), kuifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Simba ilishinda 7-0.
Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao.
Mshambuliaji wa Simba, Juma Luizuio, akimtoka kipa wa Ruvu Shooting, Bidii Hussein katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Okwi (katikati), akimpongeza Juma Luizuio.
Mshambuliaji wa Simba, Mzamiru Yassin, (katikati), akiwatoka wachezaji wa Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja sa Uhuru
 Mshambuliaji wa pembeni wa Simba, Haruna Niyonzima, akitolewa nje baada ya kuumia katika mchezo na Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, akishangilia kwa staili ya aina yake.
Emmanuel Okwi, akishangilia kwa staili ya kumshukuru mungu.
 Emmanuel Okwi akipongezana na wenzake.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanue Okwi, akimpiga chenga kipa wa Ruvu Shooting, Bidii Hussein na kuipatia timu yake bao la kwanza.
Wachezaji wa Simba wakiomba dua kabla ya mchezo kuanza.

No comments:

Post a Comment

Pages