Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii mpya kwa ajili
ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young Africans katika mchezo
kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23,
mwaka huu.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
MAJINA 8 YAPITA MCHUJO WA AWALI UONGOZI TPLB
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza
majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania
nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI DAR
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Wachezaji
wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi kutoka nje ya
mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na Elias Maguli.
Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
KAMATI YA NIDHAMU KUKETI KESHO
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya
Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, kinatarajiwa kuketi kesho Jumatato Agosti
30, mwaka huu.
Kamati hiyo itakuwa na ajenda kadhaa ikiwamo ya mashauri yanayohusu wachezaji mbalimbali, viongozi na klabu.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
No comments:
Post a Comment