HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2017

WALLACE KARIA RAIS MPYA TFF

 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallence Karia baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho.

Dodoma-Tanzania

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi wapya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya kukamilika kwa uchaguzi.

Rais mpya wa shirikisho  hilo ni Walace Karia ambaye ameibuka mshindi baada ya kushinda kwa kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.

Katika kinyang'anyiro hicho Karia alikuwa akichuana na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT, Fredrick Mwakalebelawakiwania nafasi ya urais wa TFF.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa Makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.

Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF. 
Rais wa TFF-Wallace Karia
Makamu wa Rais- Michael Wambura
Kanda 1: Saloum Chama
Kanda 
2: Vedastus Lufano  
Kanda 3: Mbasha Matutu  
Kanda4: Sarah Chao  
Kanda 5: Issa Bukuku 
 Kanda 6: Kenneth Pesambili 
 Kanda 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
 
Kanda 9: Dunstan Mkundi
 Kanda 10: Mohamed Aden 
 Kanda 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya

No comments:

Post a Comment

Pages