HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2017

Zanzibar yapongeza TAA kushirikishwa TBIII

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Ujenzi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar wakati wa ziara ya kujifunza katika ujenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi (mwenye tai nyekundu) akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Mazingira ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kushoto kwa Bw. Msangi ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar, Bw. Mohamed Ahmada Salum.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi aliyesimama akitoa maelezo ya ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi,, Mawasiliano na Mazingira ya Zanzibar walipotembelea jengo hilo.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakati kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Mazingira ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipotembelea leo kujifunza mambo mbalimbali.
Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Mazingira ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakitembelea mradi wa jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi, akitoa maelezo katika ziara ya Kamati ya Ardhi, Ujenzi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar, jijini Dar es Salaam.

Na Neema Harrison, TUDARCO

KAMATI ya Ardhi, Mawasiliano na Mazingira ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, imepongeza kushirikishwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Hamza Hassan Juma alitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea jengo hilo, na kupata maelezo na ufafanuzi mzuri kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Bw.. Salim Msangi, ambayo yanaonesha kwa kiasi kikubwa wameshirikishwa.

“Hongereni sana kwani huu mradi ni tofauti kabisa tumeona maelezo yako yanaonesha ni kwa kiasi gani mmeshiriki kuanzia mwanzo wa ujenzi hadi sasa unakaribia kumalizika, ni tofauti nakwetu siku ya mwisho ndio tunakabidhiwa mradi na tunakuwa hatujui chochote zaidi ya kukabidhiwa tu,” amesema Bw. Juma.

Naye Bw. Msangi amesema ndani ya mradi huo kumekuwa na wahandisi wa idara mbalimbali ikiwemo ya umeme walioanza tangu mradi unaanza ili baada ya mradi kukamilika inakuwa rahisi na kutambua eneo litakalokuwa na tatizo kwa ajili ya marekebisho.

Amesema katika ziara hiyo wameweza kujifunza kutoka kwa Wawakilishi hao ikiwa ni njia ya kupeana uzoefu na chachu ya maendeleo katika Viwanja Vya Ndege, ambapo katika jengo hilo kuna mifumo ya ukaguzi wa mizigo hatua tano, na endapo mzigo utakuwa na tatizo unazuiwa kwa ukaguzi zaidi katika hatua ya mwisho.

“Hii mifumo ni ya kisasa zaidi kwani hata kama abiria akiona mzigo alioweka na hauruhusiwi kupita kwenye kiwanja chetu, asidhani atakuwa amesalimika katika hatua ya tano atazuiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema Bw. Msangi.

Pia amesema jengo hilo litakuwa mitambo maalum utakayowatambua kirahisi abiria watakaokuwa wakisafirisha madawa ya kulevyia wakiwa wameyameza, ambapo awali ilikuwa rahisi kuwatambua kutokana na utaalam walionao maafisa usalama.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar, Bw. Mohamed Ahmada Salum amezungumzia kuwa TBIII itatoa ajira kwa wwatanzania wengi .

Bw. Salum amesema JNIA itarajie mashirika mengi ya ndege kujitokeza kwa wingi kufanya safari zake, na zitaongeza pato la taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages