NA FRANCIS DANDE
FAINALI ya mashindano ya hisani ya mbio za mbuzi 2017 yanatarajiwa kufanyika Septemba16 eneo la Green Oysterbay, Barabara ya Kenyatta Drive jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyeviti wa Kamati ya mashindano ya hisani ya mbio za mbuzi 2017, Rachel Carlin, alisema kuwa
‘Lengo la mashindano hayo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi ndogondogo za ndani ambazo zinajishughulisha katika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ambazo zitatumia fedha hizo katika kufanikisha kazi zao muhimu na endelevu na kuinufaisha jamii kwa upana zaidi kulingana na mahali wanapohudumu’
aliongeza kuwa ujumbe wa mashindano hayo kwa mwaka huu utakuwa ni ‘Let’s Goat Around the World’.
Alisema kuwa wao kama waandaaji, wanatumaini mbio za mwaka huu zitakuwa za mafanikio kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita ili kuongeza fedha za mfuko.
“Sisi sote tupo tayari kwa ajili ya mbio za mwaka huu na tunamatumaini ya kuwa fainali za mashidano ya mbio hizi za mwisho zitamalizika kwa mafanikio makubwa. Tunashukuru wadhamini wetu, wapya na wale wa zamani kwa kuonyesha dhamira na kusaidia mashindano haya ya mbuzi ya mwaka huu.”
Pia alitumia fursa hiyo kutambua na kuwashukuru wadhamini wakuu wa mashindano hayo ambao ni pamoja na Southern Sun Hotel, Tanzania Breweries Limited(TBL) , Coca-Cola (Kwanza), Stanbic Bank, Toyota Tanzania pamoja na SWISS International Airlines.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko Coca-Cola Kwanza, Nalaka Hettiarachchi alisema kampuni hiyo kusaidia matukio ya hisani kama haya ni miongoni mwa shughuli zake muhimu ili kuhakikisha wanajenga jamii iliyo imara.
Alisema Mbio za Mbuzi ni sehemu ambayo inaweza kuhimiza jamii katika kushiriki masuala ya kijamii yanayoandaliwa ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya kijamii na uchumi.
Milango ya eneo la mashindano hayo ya hisani ya Mbio za mbuzi inatarajiwa kufunguliwa kuanzia 6 mchana na kufungwa saa 11:15 jioni.
No comments:
Post a Comment