Kamati ya Bunge ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge, imeahirisha kumuhoji Mbunge wa Jimbo la Ubungo,
Mhe. Saed Kubenea kutokana na kufika mbele ya Kamati hiyo akiwa mgonjwa.
Mhe. Kubenea alifika
mbele ya Kamati majira ya saa 4 asubuhi akiwa katika baiskeli ya wagonjwa ya miguu
minne (Wheel chair) chini ya ulinzi wa Askarii wa Jeshi la polisi.
Akizungumzia katika kiao
hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Kapteni
Mstaafu George Mkuchika alisema kamati hiyo imekutana kutokana na kuletewa
shauri na Mhe. Spika la kumuita Mbunge huyo kwa madai ya kudharau mamlaka ya
Spika kwa kauli alizozitoa katika kanisa moja Jijini Dar es Salaam.
“Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
inakutana pale inapoletewa shauri na Mhe. Spika, tumeletwa mashauri ya Mhe.
Kubenea, ya kudharau Mamlaka ya Spika kwa kauli ambazo amezitoa katika kanisa
la huko Dar Es Salaam,” alisema.
Alisema taratibu
zinamtaka mtu anayetakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kupelekewa Hati ya kuitwa
na kwamba alishapelekewa.
Alisema hata hivyo Mhe.
Kubenea amepelekwa akiwa katika baiskeli ya wagonjwa na kuiomba Kamati impangie
siku nyingine na kwamba Kamati hiyo imeridhia ombi lake.
“Kamati baada ya
kumsikliza Mhe. Kubenea imeridhia ombi lake la kumpangia tarehe nyingine kwa
kumpa muda wa kuangalia afya yake mpaka atakapopona,”
alisema.
alisema.
Mhe. Mkuchika aliagizaa
Mhe. Kubenea apelekwe katika Zahanati ya Bunge ili aweze kupewa huduma ya
kwanza.
Awali Mhe. Kubenea baada
ya kuhojiwa na kamati kama ataweza kuzungumza katika kikao hicho aliiomba
kamati kumpangia siku nyingine kwa kuwa asingeweza kuzungumza kwa wakati ule
kutokana na kuwa katika maumivu makali.
Septemba 12, mwaka huu,
Mhe. Spika Job Ndugai aliagiza Mbunge huyo kufika mbele ya kamati hiyo kwa kuhojiwa
kuhusiana na tuhuma alizozitoa wakati wa Ibada tarehe 10 Septemba, 2017 kwamba
Mhe. Spika alisema uongo Bungeni wakati akitangaza idadi ya risasi zilizopigwa
kwenye gari la Mhe. Tundu Lissu.
Mhe.
Spika pia aliiagiza Kamati hiyo Mhe.
Zitto Kabwe kufuatia kauli zake alizozitoa kwenye mitandao kwamba Mhimili wa
Bunge umewekwa mfukoni na Serikali na kwamba Bunge lilikosea kushughulikia
Taarifa za Kamati kuhusu Almasi na Tanzanite.
No comments:
Post a Comment