HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 21, 2017

UKAGUZI WA KINGA NA TAHADHARI YA MOTO KWA VYOMBO VYA USAFIRI NA USAFIRISHAJI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapenda kuutangazia umma kwamba linaendelea na zoezi la ukaguzi wa vyombo vya Usafiri na Usafirishaji. Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni ya Usalama na Vyeti ya Mwaka 2008 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012 na 2014.

Huduma hii ya ukaguzi wa vyombo vya Usafiri na Usafirishaji inatolewa bure, hii ni baada ya Serikali kuondoa tozo ya ukaguzi wa vyombo hivi iliyokuwa ikitozwa pale ambapo mmiliki alipokuwa akienda kukata ushuru wa barabara “Road license’’ kuanzia mwaka wa fedha wa serikali 2017/2018. Ukaguzi huu unazingatia uwekaji wa vifaa vya uzimaji moto katika vyombo hivyo pamoja na utoaji wa elimu ya kinga na tahadhari ya moto kwa watumiaji.

Jeshi linatoa rai kwa wananchi wote kupeleka magari yao katika vituo vya Zimamoto vilivyopo karibu ili kupata huduma hii, HUDUMA HII NI BURE na ni kwa USALAMA WAKO MWANANCHI.

Iwapo utapata huduma hii kwa kutozwa fedha yeyote tafadhali wasiliana na Kamanda wa Mkoa husika, kwani ni kinyume na utaratibu.

Imetolewa na;
 
Ofisi ya Habari na Elimu kwa Umma

Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji


20 Septemba, 2017

No comments:

Post a Comment

Pages