Kampuni Tigo Tanzania
imetambulisha huduma mpya ya Tigo Business inayotoa bidhaa na huduma mahsusi
kwa biashara na mashirika ya aina yote ili kuongeza ufanisi, ukuaji na faida.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari,
alisema kuwa Tigo Business inatoa huduma za kipekee zinazolenga mashirika ya
umma, serikali, biashara binafsi, kampuni za usambazaji na usafirishaji,
mashirika ya fedha, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wachimbaji madini,
viwanda na kadhalika; huku ikiwapa uhuru wa kufanya shughuli zao kwa ueledi
zaidi na kuwawezesha kufanikisha miradi yao nchini na nje ya nchi.
‘Tigo Business ndio huduma
ya mawasiliano ya biashara inayokuwa kwa kasi zaidi nchini. Inajumuisha
biashara za aina zote bila kutegemea ukubwa wa biashara au bajeti, huku ikiwapa
wafanyabiashara amani na uhuru wa kushugulikia masuala ya muhimu zaidi
yanayohusu ukuaji wa biashara zao,’ Karikari alisema.
Tigo Business inafanikisha
mahitaji tofauti ya mawasilano ya biashara ikiwemo mawasiliano ya sauti, data
na mifumo ya mitambo ya biashara kwa ufanisi wa juu na kwa gharama nafuu zaidi.
Kwa kutumia uwekezaji mkubwa wa
Tigo katika mkongo wa mawasiliano (fibre) na
kituo cha kuhifadhia kumbukumbu (data centre), Tigo business imejikita
kuongoza soko la mawasiliano ya kisasa ya biashara huku ikiboresha jinsi wateja
wanavyotumia mawasiliano ya kisasa.
‘Tigo Business inaelewa kuwa
dunia ya sasa imeunganishwa kwa mtandao na hii inabadilisha jinsi biashara
inavyofanyika. Kwa kutumia mtandao wetu
na bidhaa zetu, Tigo inatumia uzoefu
wetu wa maisha ya digitali kuleta mageuzi katika mifumo ya biashara,’ Karikari
alisema.
No comments:
Post a Comment