Wajumbe kutoka
Ujerumani waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na
nchi hiyo wakisililiza kwa makini maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani) akieleza mafanikio ya msaada
wa nchi hiyo katika Nyanja za Afya, Maji, Nishati na Utawala wa Fedha, katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi
kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo
kati ya Tanzania na Ujerumani yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Wachter (wa pili kushoto)
akizungumza kuhusu nia ya nchi yake kuisaidia Tanzania katika miradi ya
Nishati, Maji, Utawala wa Fedha na Afya kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo
kuanzia mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) na
Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka
Ujerumani Bw. Georg Rademacher
wakibadilishana kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano baada ya kusainiwa katika
Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nne kushoto) na
Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka
Ujerumani Bw. Georg Rademacher
(kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Ujerumani
na Tanzania baada ya kusainiwa kwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano, katika
ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi
wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba
akipeana mkono na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa Kiuchumi Kanda ya Afrika
Mashariki kutoka Ujerumani Bw.
Georg Rademacher (kushoto) baada ya kusainiwa kumbukumbu za Mkutano wa
Mashauriano ya Maendeleo kati ya nchi hizo mbili Jijini Dares Salaam. (Picha na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Ujerumani
imeipatia Tanzania kiasi cha Euro milioni 198.5 sawa na Sh. Bilioni 520.86 zilizotumika kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo
ya Maliasili na Mazingira, Afya, Maji, Nishati, Udhibiti wa Fedha za Umma (Good
Financial Governance) na Kusaidia Huduma za Wakimbizi katika mkoa wa Kigoma,
katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban wakati wa tukio la Tanzania na Ujerumani kusaini
kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo (Bilateral Development
Consultations) ambapo Ujerumani imeonesha nia ya kuendelea kuisaidia Tanzania
katika Sekta hizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021.
Kumbukumbu za
Mashauriano hayo zimesainiwa na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Naibu Mkuu wa Idara ya Kanda ya Afrika Mashariki katika Wizara
ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Bw. Georg Rademacher kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani.
Mkutano
huo ni maandalizi ya mkutano wa Majadiliano ya Kimaendeleo (Bilateral
Negotiations) kati ya nchi hizi mbili unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018 ambapo
Serikali ya Ujerumani itatangaza kiasi cha fedha watakazotoa kama msaada kwa
ajili ya kufadhili Sekta zilizoainishwa katika kumbukumbu zilizosainiwa.
“ Tunaishukuru
Ujerumani kwa kuwa miongoni mwa washirika wa muda mrefu wanaotoa misaada
mikubwa ya kimaendeleo kwa Tanzania na sisi tunaahidi kuendeleza ushirikiano
huo kwa faida ya pande zote mbili” alisema Bi. Amina Khamis Shaaban.
Kwa upande wake Bw. Georg Rademacher kwa niaba ya Serikali ya
Ujerumani amesema kwamba Tanzania imekuwa na sifa njema nchini Ujerumani hasa
kwa sababu ya amani iliyopo, jinsi ambavyo imehifadhi maliasili zake na
kuifanya kuwa nchi yenye vivutio vya kipekee vya utalii.
Bwana Rademacher aliongeza kwamba kwa sasa nchi ya
Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika kupambana na ubadhirifu wa mali za
Umma na kwamba Ujerumani itaendelea kuisaidia Tanzania ili kuweza kuleta
maendeleo kwa watu wake na kuondoa umaskini.
Imetolewa
na;
Benny
Mwaipaja
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Fedha na Mipangowa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment