HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 31, 2017

BENKI YA CRDB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA MEWATA

Meneja wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB tawi la Oysterbay, George Abraham, akitoa mada kuhusu huduma mbalimbali zilinazotolewa na benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (Mewata).  
Oisa Uhusiano Mwadamizi wa Benki ya CRDB, Alma Laay, (kulia), akimpa maelezo kuhusu akaunti ya Malkia mmoja wa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (Mewata), uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya CRDB.
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa Mewata. 
Dk. Grace Kaw, akichangia mada katika mkutano huo.
Meneja wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB tawi la Oysterbay, George Abraham, akitoa ufafanuzi kuhusu akaunti ya Malkia kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (Mewata).  
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Florene Mbolii (katikati), akitoa maelezo kwa mmoja wa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA), namna anavyoweza kunufaika na akaunti ya Malkia ya benki ya CRDB, uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.  Kulia ni Ofisa wa benki hiyo, Clementine Shao na wa pili kushoto ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Mary Mwakalukwa.


No comments:

Post a Comment

Pages