HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 26, 2017

KESI YA LULU KUENDELEA OKTOBA 26

NA MWANDISHI WETU

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na washauri waungwana wa mahakama hiyo wanatarajia kutoa muhtasari wa kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Jana Jaji Sam Rumanyika alisema  kuwa muhtasari huo utasaidia wazee wa baraza kupitia shauri hilo kuamua kama Lulu anahatia ama la baada ya kufungwa ushahidi wa pande zote mbili.

Akisoma maelezo ya mushumbusi, Askari Polisi E 103, Sajenti Nyagea (53), Alidai Mshumbuzi alimwambia kuwa yeye ni mmiliki ya clinic ya tiba mbadala iliyopo katika jengo la Mawasiliano barabara ya Sam Nujoma.

Amesoma kuwa katika clinik yake alikuwa na Wateja wa aina mbali mbali akiwemo marehemu Steven Kanumba ambaye alimfahamu tangia Agosti mwaka 2011 alipofika katika clinic yake hiyo kwa Mara ya kwanza kwa ajili ya kutoa sumu mwilini. Na kuanzia hapo akawa na mazoea ya kwenda pale clinic kwa ajili ya Huduma hiyo.


Shahidi Nyangea ameeleza kuwa, Kanumba alikuwa akienda pale na alikuwa anapima afya yake kwa kutumia machine kuchunguza mwili wake wote.

Amedai katika Maelezo yake Mshumbuzi alidai kuwa Kanumba aligundulika kuwa na mafuta (colestro) na tatizo la moyo Heart attack) na upungufu wa hewa ya oxygen kwenye ubongo.

" Matatizo hayo yalimletea udhaifu wa mwili mfano alikuwa na maumivu makali ya moyo, mara kwa mara alikuwa akichoka.

Katika matibabu yake alidai aligundua kuwa Kanumba alikuwa anafanya mazoezi ya kutanua misuli ambapo alimshauri aachane na mazoezi hayo kwa muda sababu mzunguko wake wa damu haukuwa mzuri na ungeweza kumpelekea sababu za kifo au kupooza.

"Ili ujue MTU amekufa kwa kupoteza hewa misuli yake hubadilika rangi na kuwa ya bluu" ilidai repoti hiyo.
Ameendelea kueleza, siku chache baada ya ushauri wake huo kwa Kanumba, alisikia kuwa amefariki.

"Alinieleza anamaumivu makali yanamuumiza sana moyo lakini hakumwambia ni tatizo gani, aliniomba nimpe ushauri nasaha, lakini sababu nilikuwa na Wateja wengi na muda haukutosha tulipanga tukutane siku nyingine lakini Bahati mbaya hakuweza kupata nafasi hiyo kwani alisikia Kanumba amefariki.

 Shahidi huyo amedai, baada ya kumaliza kurekodi maelezo ya Mshumbusi, aliyapeleka ofisini kituoni hapo na akaambiwa ampe sajenti Ernatus ambaye ndio alikuwa mpelelezi wa  kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages