Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna
Mgwhira akihutubia washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya
kiwanda cha kuchakata tangawizi kilichopo wilayani Same ambapo Mfuko wa
Pensheni wa LAPF umewekeza ili kiwanda kianze uzalishaji. Hafla hiyo ilifanyika
tarehe 28/09/2017.
Meneja wa Uwekezaji na Mipango wa Mfuko wa
Pensheni wa LAPF Bw. Furtunatus Magambo ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi ya
Kiwanda cha kusindika tangawizi akizungumza na wajumbe pamoja na wageni
waalikwa kwenye hafla ya kuzindua Bodi iliyofanyika wilayani Same, mgeni rasmi
akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mgwhira.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano
wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari
baada ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha kusindika tangawizi
kilichopo wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Kushoto ni Meneja wa Miradi na
Miliki wa LAPF Eng. Greyson Bambanza ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya kiwanda
hicho ambacho LAPF inawekeza kiasi cha Shs. Bilioni moja.
No comments:
Post a Comment