Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiangalia picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake wakati alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, kabla ya kuzizindua jijini Dar es Salaam jana. Walioshika bango lenye picha za stempu hizo kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (wa pili kulia), akimueleza jambo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi (kulia), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, baada ya uzinduzi wa stempu hizo.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mara baada ya uzinduzi huo.
TAREHE 12 Oktoba, Mkuu wa Taasisi ya
Agha Khan Foundation, Mtukufu Karim al-Hussayni
Agha Khan ambaye pia ni kiongozi Mkuu wa Jumuia ya Ismailia duniani na
mtu anayeheshimika sana hasa kwa jamii ya Kihindi, alizuru nchini Tanzania na
kufanya shughuli mbali mbali za Kitaifa na kibinafsi nchini.
Pamoja na kuwa na manufaa makubwa kwa
nchi pia ziara hiyo ilikuwa muhimu sana kwa Shirika la Posta Tanzania.
Mbali na kutembelea miradi mbali
mbali inayofadhiliwa na taasisi yake, alipata fursa ya kuzindua stampu zilizochapishwa
na Shirika la Posta zinazoelezea au kuonyesha kumbukumbu muhimu za taasisi ya
Agha Khan.
Uzinduzi wa stampu hizo ulifanyika
kwenye ukumbi wa uwanja wa ndege wa mwl.nyerere akiwa njiani kurudi ,baada ya
ziara yake hapa nchini kukamilika.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Dk. Hussein Mwinyi kwa niaba ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Dk. John Joseph Pombe Magufuli ndiye aliyemkabidhi stampu hizo kutoka kwa Kaimu
Postamasta Mkuu bw.Macrice Mbodo.
Stampu hizo, zenye kumbukumbu maalum
za Agha Khan ni pamoja na jengo la dispensary ya zamani iliyojengwa na taasisi
ya Agha Khan mjini Unguja pamoja na za picha za shughuli mbalimbali za kijamii
zilizofadhiliwa na taasisi hiyo.
Uchapishaji wa stampu hizo,
ulidhaminiwa na taasisi hiyo, kwa gharama ya shilingi milion 52, zikiwa ni
stempu maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya Diamond Jubilee- miaka 60 ya tangu
kusimikwa kwake kuwa Imamu Mkuu wa dhehebu la Shia Ismailia.
Mwaka 2007, taasisi ya Agha Khan
waliweza pia kufadhili uchapishaji wa stampu maalum za kuadhimisha Golden
Jubilee (1957-2007), kwa kiasi cha dola 10,573.24 .Stampu hizo zilikuwa na
dhamani ya shilingi 267,059,000/=
Stampu hizo zitaweza kutumika kwa
ajili ya matumizi ya kawaida (postage) na zaidi kwa wakusanya stampu (stamps collectors),
ambao mbali na kuweza kuzipata kupita kaunta za Posta na mawakala wa stampu,
pia kwa sasa wanaweza kuzipata kupitia duka maalum (online) ambalo limeanzishwa
na shirika la Posta.
Mteja yeyote akiwa popote Duniani
anaweza kununua kupitia Web site ya Posta, ambapo ataingia kwenye kipengele cha
e-busness na bonyeza e-service, kisha e-shop na atapata aina mbalimbali za
stampu na maelekezo ya namna ya kununua.
No comments:
Post a Comment