HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 26, 2017

Sekondari Tanga Zapata Elimu Kwa Njia ya TEHAMA Tigo yatoa msaada wa mfumo wa elimu kwa njia ya mtandao kwa shule mbili za sekondari

Tanga 25 Oktoba, 2017
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania kupitia mradi wake wa Tigo E-schools imezidi kuleta mageuzi makubwa ya elimu nchini baada ya kutoa msaada wa mfumo wa elimu kwa njia ya mtandao kwa shule ya Sekondari Shemsanga na Sekondari ya Handeni zilizopo Mkoani Tanga. 

Tigo E-schools pia inasambaza mfumo huo wa elimu kwa jumla ya shule 52 za sekondari katika mikoa 12 ambayo msimu wa Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa utazuru mwaka huu.

Ikiwa ni sehemu ya shughuli za jamii zinazoendana na msimu wa Tigo Fiesta 2017Tumekusomaa,  kupitia mradi wa Tigo e-schools, Tigo imeona na kuelewa hitaji la wanafunzi la maarifa ya Tehama, na inakutana na hitaji hili kupitia  utoaji wa kompyuta zilizounganishwa na intaneti na mifumo mbali mbali ya elimu. 

Hafla fupi ya kukabidhi mfumo huo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Tigo – Kanda ya Pwani, George Lugata alisema kuwa msaada huo unaonesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa wateja wake na kuwapa huduma zinazoendana na mahitaji yao.

‘Dunia ya sasa inaendeshwa kidigitali. Mradi wa Tigo E-shools unawaandaa wanafunzi kuwa sehemu ya ulimwengu huu wa kidigitali. Mfumo huu wa elimu kwa njia ya mtandao utawaandaa wanafunzi kuwa sehemu ya mabadiliko ya Tehama ulimwenguni. Wanafunzi wataongeza busara, kupanua mitazamo na ubunifu wao, na hivyo kuibua fursa pamoja na kukabiliana na changamoto zinazoendana na ulimwengu wa sasa wa digitali,”  Lugata alisema.

Meneja huyo wa kanda alifafanua kuwa mwaka 2016, Tigo ilifanya makubaliano na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwezesha kusambazwa kwa mtandao katika shule za sekondari nchini ili kuchangia mpango wa miaka miwili wa serikali kuleta mabadiliko ya elimu kwa njia ya mtandao.
Kama sehemu ya makubaliano hayo, Wizara ilitoa majina ya shule zisizokuwa na maabara ya kompyuta na pia kutoa mwongozo wa utekelazaji wa mradi huo. Tigo ilishiriki katika ujenzi na kuunganisha maabara mpya za kompyuta na mtandao, na hatua ya tatu ni ya kuunganisha shule husika na teknologia hii ya elimu kwa njia ya mtandao.

“Kupitia mpango wetu endelevu wa kuwekeza katika hudma za jamii, Tigo inachangia jitahada za serikali za kuigeuza Tanzania kuwa na uchumi wa maarifa ifikapo mwaka 2025.”  Lugata aliongeza.

Shule nyingine ambazo tayari zimeunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama ni Arusha Day, Ilbouru na Arusha Sekondari mkoani Arusha na Sekondari za Mwanza, Pamba na Mirongo zilizopo mkoani Mwanza.

Shule nyingine ambazo zimeunganishwa na mfumo huo wa kisasa wa elimu ni shule za Iringa na Kleruu Sekondari mkoani Iringa; Matalawe na Songea Girls Sekondari mkoani Songea; Njombe na Mpechi Sekondari mkoani Njombe;

Shule ambazo sipo mbioni kuunganishwa na mfumo huo ni Mpwapwa Sekondari mkoani Dodoma, Morogoro Municipal na Mzumbe Sekondari zilizopo Morogoro; Lyamungo Sekondari na Machame Girls Sekondari huko Moshi; Newala Day na Masasi Day Sekondari zilizopo Mtwara na kwa mkoa wa Dar es Salaam, sekondari za Mbagala, Kibamba, Benjamin Mkapa na Makumbusho zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama.

Kwa niaba ya Serikali natoa shukurani za dhati Tigo Tanzania kuwa sehemu ya mipango yake ya kuiingiza Tanzania katika mfumo wa uchumi wa maarifa. Ni matumaini yangu kuwa wanafunzi watatumia fursa hii kujiendeleza kitaaluma ili wawe sehemu ya ulimwengu wa sasa unaotegemea TEHAMA katika uendeshaji wake,’ Mkuu wa Mkoa wa Tanga .

Tigo ni mdau muhimu wa elimu na imetoa michango mbali mbali kuinua viwango vya elimu nchini. Mwaka jana Tigo ilichangia madawati zaidi ya 7,100 katika shule za mzingi nchini kote. Vilevile Tigo imetoa kompyuta 77 zilizounganishwa na mtandao wa kasi zaidi wa Tigo kwa vituo vya elimu ya juu nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela akitoa hotuba katika uzinduzi wa mfumo wa elimu unaotoa masomo 11 ya shule kwa njia ya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Handeni, mkoani Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe Godwin Gondwe na kushoto ni Meneja wa Mahusiano ya Serikali wa Tigo, Halima Okash.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martin Shigela akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo unaotoa elimu kwa njia ya TEHAMA, Tigo E-schools uliotolewa na kampuni ya Tigo katika shule ya Sekondari ya Handeni, Mkoani Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe Godwin Gondwe na kushoto ni Meneja wa Mahusiano ya Serikali wa Tigo, Halima Okash. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martin Shigela (kushoto),  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe Godwin Gondwe, (kati) na Meneja wa Mahusiano ya Serikali wa Tigo, Halima Okash (kulia) wakipata maelezo kuhusu  mfumo unaotoa elimu kwa njia ya TEHAMA uliotolewa na kampuni ya Tigo kupitia mradi wa Tigo E-schools kwa shule ya Sekondari ya Handeni, Mkoani Tanga leo. Jumla ya shule 52 za sekondari nchini zitaunganishwa na mfumo huo unafundisha masomo 11 kwa njia ya digitali.

No comments:

Post a Comment

Pages